Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya vyeti watakavyopewa kinamama walioshinda shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International. |
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” |
Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo. |
Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo. |
- Itashirikana na REPOA, CARE INTERNATIONAL & KIDOGO
KIDOGO
Rufiji, Desemba 23, 2015: Tigo imetoa simu za mkononi 200 ambazo
zitasambazwa kwa wanawake maskini ambao hawana uwezo wa kununua simu katika
wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, lengo kuu likiwa ni kuziba pengo la kijinsia
katika umiliki wa simu Tanzania.
Usambazaji wa simu hizo upo chini
ya programu inayojulikana, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” utafanyika kwa
kushirikiana na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care
International.
Akizungumzia zoezi hilo Meneja
Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, alisema kwamba mtazamo wa Tigo uko kwenye
sera za kampuni ya kuwawezesha watu walio na kipato duni ndani ya jamii katika
kuzipata simu za mkononi.
“Tigo inadhamiria kuboresha muunganisho wa simu za
mkononi nchini Tanzania hususani
miongoni mwa wanawake ambao kimsingi
wana uwezo mdogo wa kupata simu,” alisema Bi.Thomas na kuongeza, “Ni matumaini
yetu kwamba kwa kusambaza simu hizi kwa
wanawake maskini katika wilaya ya Rufiji, Tigo itakuwa imechangia
kupunguza pengo la kijinsia katika
umiliki wa simu nchini.”
Thomas alisema kwamba Tigo imewekeza zaidi ya
dola 30,000 ambazo zitatumika kusambaza
pamoja na kuangalia tathmini ya matokeo ya mradi. Aliongeza kwamba
washirika watatu REPOA, CARE International na KIDOGO KIDOGO kwa pamoja
wataongoza utekelezaji huo wa usambazaji wa simu kwa kutoa laini ya simu pamoja
na kufanya tathmini ya matokeo ya mradi.
“Pengo lililopo la kijinsia
katika kuifikia teknolojia ya simu linaweza kukwaza Tanzania katika mchakato wa
kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika kukuza usawa kijinsia na
kuwawezesha wanwake nchini na ndio maana Tigo inachukua hatua za kuunga mkono
mradi huu,” alisema Bi.Thomas.
Kwa mujibu wa Bi. Thomas mradi huo unalenga
kuwanufaisha watu 500 katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 na inakuwa ni mara
ya pili kwa Tigo kusambaza simu za
mkononi kwenye mkoa huo kwani mara ya kwanza ilikuwa amwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment