Waziri
Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia)
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba
wakati wa mapokezi yake tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya
Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu. Nyuma yake kulia ni naibu
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho
katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
Waziri
Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini
kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya
iliyopo Mpingo House tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari
wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru
(kushoto).
Waziri
Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri
Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni
ofisini kwake tarehe 28 Desemba 2015.
Picha
ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne
Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa
pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza
kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto).
Sehemu
ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa
mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa
Ikulu na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe
Magufuli.
(Picha na Hamza Temba – Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)
0 comments:
Post a Comment