Mvuvi
Waziri Mfaume ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam
alikutwa na mpiga picha leo akishimba shimo kwa ajili ya kuhifadhia
uchafu kandokando ya barabara ya Barrack Obama ambayo zamani ilifahamika
kwa jina la barabara ya bahari (Ocean Road). Anayeonekana akifagia eneo
hilo ni Mama Chiku Hamadi Mkazi wa Mwananyamala.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan
Mmbando akiongea na waandishi wa Habari waliofika katika soko la samaki
la Feri jijini Dar es Salaam kuona jinsi usafi wa mazingira ulivyokuwa
unafanyika sokoni hapo.
Makatibu
wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt .Donan Mmbando (wapili
kulia) na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Ndg. Jummanne Sagini (watano kulia) wakifanya usafi katika
Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam. Wengine walioshirikia kazi
ya kufanya usafi ni wafanyakazi wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando akiongea na
wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kumalizika kwa kazi ya kufanya
usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa wizara hiyo walifanya usafi katika mahabusu ya watoto
Kisutu, Makazi ya Wazee ya Nunge, Taasisi za Mifupa MOI na Saratani ya
Ocean Road, Hospital ya Taifa Muhimbili, Masoko ya Kariakoo na Feri, na
Mbagala Zakhem.Wafanyakazi
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa na nyuso za furaha mara
baada ya kumaliza kazi ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo
mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa wizara hiyo walifanya
usafi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifanya usafi wa
mazingira leo katika soko la samaki la Feri ikiwa ni kutekeleza agizo la
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufanyika kwa usafi wa mazingira
nchi nzima ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
0 comments:
Post a Comment