Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa tatu
kulia) akielekea eneo la kufanya usafi kuzunguka maeneo ya ofisi za
wizara hiyo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa
agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya
sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha
Deodata Makani akitoa maelekezo ya kufanya usafi kuzunguka ofisi za
Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watumishi wakikata matawi ya miti kwa makini bila
kuharibu nya za simu yaliyokuwa kizuizi katika barabara eneo la ofisi za
wizara ya fedha kwa lengo la kufanya usafi leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiendelea
kufanya usafi katika moja ya sehem ya kuzunguka maeneo ya ofisi za
wizara hiyo leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa
agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya
sherehe za Uhuru mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na
watumishi wa wizara hiyo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliza
zoezi la kufanya usafi ikiwa ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la
kufanya usafi katika eneo ya kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za
Uhuru mwaka huu.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile leo
ameiongoza wizara hiyo katika kuitikia na kutekeleza agizo la Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya
usafi katika eneo lao la kazi katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru ya
mwaka huu.
Akiongea na watumishi wa Wizara hiyo, Dkt. Likwelile alisema kuwa
maadhimisho ya siku ya uhuru yaendelee kutumika kama kichocheo cha
kujenga tabia ya kufanya kazi ikizingatiwa dhana iliyokuwepo tangu uhuru
ilikuwa “Uhuru na Kazi” ambapo kwa sasa kaulimbiu ya Rais Dkt. Magufuli
inasema “Hapa Kazi Tu”
“Ni uamuzi mzuri wa Rais, ni wa busara na unaendana na tulipotoka
ambapo Tanzania inaamini katika “Uhuru na Kazi”, huu ni mwanzo wa
kusimama kwa miguu yetu wenyewe ili kujiletea maendeleo kwa kuendelea
kuwapiga vita maadui watatu wa taifa” alisema Dkt. Likwelile.
Dkt. Likwelile aliwataja maadui hao kuwa ni ujinga, maradhi na
umasikini ambao ndiyo wamekuwa chanzo cha kurudisha nyuma juhudi za
maendeleo, kwa kuimarisha suala la usafi katika mazingira yote nchini,
itakuwa mwanzo wa kupambana na suala magonjwa milipuko ikiwemo
kipindupindu ambao asili yake ni uchafu.
Aidha, Dkt. Likwelile aliwaasa watumishi wa wizara hiyo na
Watanzanaia kwa ujumla kuenzi kazi iliyonzishwa na Mhe. Rais Dkt.
Magufuli ya kufanya usafi na zoezi hilo liwe endelevu na la kudumu
ambapo ameahidi kuwa wizara yake itapanga siku ya kufanya usafi mara kwa
mara katika maeneo ya kazi ili kudumisha usafi ambao ni suala muhimu
katika kuimarisha afya zao na ikizingatiwa watumishi hutumia muda mwingi
wakiwa katika maeneo ya kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DHRM)
Wizara ya Fedha Deodata Makani alisema kuwa mwitikio wa watumishi katika
zoezi la usafi umekuwa mkubwa na wanapendekeza zoezi hilo liwe endelevu
maana watumishi hutumia muda mwingi katika maeneo ya kazini hivyo ni
vema kuyaweka mazingira hayo katika hali ya usafi ili yawe rafiki wakati
wote wa kutekeleza majukumu yao.
Naye mmoja wa watumishi wa Wizara hiyo William Muhoja alisema kuwa
zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya kazi linatakiwa kufanywa kila
wakati ambapo itakuwa ni sehemu ya watumishi kuwajibika kwa jamii katika
maeneo yao wanapoishi na wanapofanya kazi.
Sherehe za uhuru mwaka huu nchini zimeadhimishwa kwa namna tofauti
na ilivyozoeleka miaka iliyopita ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mamlaka aliyonayo
kikatiba alitangaza maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri ya 9
Disemba mwaka huu, Watanzania wote waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali
kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji
yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Maadhimisho hayo yanaendelea nchi nzima ambapo kila halmashauri
inatekeleza agizo la Mhe. Rais kwa vitendo kwa kufanya usafi katika
maeneo yao, zoezi linashirikisha Wizara, idara, taasisi za Kiserikali na
zisizo za kiserikali, maeneo ya viwanda, shule, vyuo, maeneo ya
biashara, masoko na kuzunguka maeneo yote ya makazi ya watu.
0 comments:
Post a Comment