WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya Uganda, The Cranes wamepata ajali iliyosababisha vifo vya watu saba jana.
Wachezaji
wa The Cranes walikuwa wanatoka wilaya ya Soroti baada ya kukutana na
Rais Yoweri Museveni walipoalikwa baada ya kutwaa taji la 14 la Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini Ethiopia
Jumapili.
Ajali
hiyo ilisababishwa na tairi la mbele la basi lililokuwa limebeba
wachezaji wa Cranes kupata pancha na kupoteza mwelekeo eneo la Mbale
katika maegesho ya teksi ya Jami mjini Kamonkoli, wilaya ya Budaka.
Basi hilo la The Cranes lilikwenda kuigonga gari ndogo ya abiria (Hiece) na kusababisha vifo vya watu saba, kwanza watatu wakifariki papo hapo. Taarifa ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) imesema wachezaji watatu Kezironi Kizito, Denis Okot Oola, Hassan Wasswa Dazo na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya FUFA, Ahmed Hussein wameumia. Ofisa wa Usalama barabarani wa Bukedi, Paul Okongo amewataja baadhi waathirika wa ajali hiyo kuwa ni Charles Mwima, Wahab Nakifuyi, Zainabu Nabusuyi na Samuel Kagulu, wakati wengine hawajatambulika. "Dereva wa basi la The Cranes ndiye anastahili lawama kwa ajali hii, kwa sababu alikuwa anaendesha kwa kasi sana," amesema Okongo. “Alishindwa kulimudu gari baada ta tairi moja kupasuka,"
Basi la The Cranes likiwa limegongana na basi dogo la abiria |
Kikosi cha The Cranes kikikuwa na Rais Museveni kabla ya kwenda kupata ajali |
Basi hilo la The Cranes lilikwenda kuigonga gari ndogo ya abiria (Hiece) na kusababisha vifo vya watu saba, kwanza watatu wakifariki papo hapo. Taarifa ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) imesema wachezaji watatu Kezironi Kizito, Denis Okot Oola, Hassan Wasswa Dazo na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya FUFA, Ahmed Hussein wameumia. Ofisa wa Usalama barabarani wa Bukedi, Paul Okongo amewataja baadhi waathirika wa ajali hiyo kuwa ni Charles Mwima, Wahab Nakifuyi, Zainabu Nabusuyi na Samuel Kagulu, wakati wengine hawajatambulika. "Dereva wa basi la The Cranes ndiye anastahili lawama kwa ajali hii, kwa sababu alikuwa anaendesha kwa kasi sana," amesema Okongo. “Alishindwa kulimudu gari baada ta tairi moja kupasuka,"
0 comments:
Post a Comment