https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    TOP 5 Stories: Debuchy anajutia kuwa Arsenal kisa?, Hiddink anataka Terry apewe mkataba, mbaya wa Taifa Stars kutua Arsenal …


    Mtu wangu wa nguvu bado headlines za dirisha dogo la usajili barani Ulaya zinazidi kuchukua nafasi, najua wengi mnataka kufahamu mchezaji yupi kaenda wapi na mwingine anatokea wapi, lakini nani yupo katika mipango na klabu fulani. January 18 nakusogezea Top 5 stories za usajili wa wachezaji soka barani Ulaya ambazo zimeingia kwenye headlines January 18.
    5- Debuchy anajutia kujiunga na Arsenal
    Beki wa kimataifa wa Ufaransa anayechezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Mathieu Debuchy anajutia kujiunga na klabu ya Arsenal ambayo kwa sasa anakosa namba, kwani beki wa kihispani Hector Bellerin anaonekana kufanya vizuri. Debuchy ambaye alianza kupoteza namba wakati yupo majeruhi, ana hofu ya kukosa michuano ya EURO 2016 itakayofanyika kwao Ufaransa.
    LONDON, ENGLAND - AUGUST 03: Mathieu Debuchy of Arsenal in action during the Emirates Cup match between Arsenal and AS Monaco at the Emirates Stadium on August 3, 2014 in London, England. (Photo by Michael Regan/Getty Images)
    4- Diego Costa anarudi Laliga
    Diego Costa anayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza anaripotiwa kuwa na mipango ya kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Atletico MadridCostaambaye toka amejiunga na Ligi Kuu Uingereza amekuwa kwenye headlines za kufungiwa kutokana na makosa yake kadhaa, ameandikwa katika mtandao wa Fichajes.net kuwa na mpango wa kurudi Hispania.
    Diego-Costa23
    3- Guus Hiddink anataka John Terry apewe mkataba
    Kocha wa muda wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Guus Hiddink ameiomba klabu yaChelsea kuwaongezea mikataba wachezaji muhimu katika timu wenye umri mkubwa kama John TerryChelsea huwa na utamaduni wa mchezaji akiwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huwa hawana mpango wa kumpa mkataba.
    john-terry-
    2- Louis van Gaal athibitisha kuwa katika mbio za kuutwa ubingwa
    Baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Liverpool, kocha wa Man United Louis van Gaalametamka kuwa kikosi cha Man United kipo katika nafasi ya kuwania ubingwa. Man United wanatajwa kuwa hawakucheza vizuri au soka safi na kuvutia hiyo siku, ila kilichokuwa kinahitajika ni ushindi dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu Liverpool.
    Louis-van-Gaal32
    1- Arsenal imetenga dau zito kwa ajili ya kumsajili mchezaji wa Leicester City
    Daily telegraph linaripoti kuwa klabu ya Arsenal kupitia mascout wake, wamepanga kufanya usajili mkubwa kutoka Leicester CityArsenal wanataka kumsajili mmoja kati ya wachezaji wa Algeria Riyad Mahrez  aliyefunga goli katika mchezo dhidi ya Taifa Stars uliyomaliazika kwa Stars kupokea kipigo cha goli 7-0.
    Riyad-Mahrez

    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TOP 5 Stories: Debuchy anajutia kuwa Arsenal kisa?, Hiddink anataka Terry apewe mkataba, mbaya wa Taifa Stars kutua Arsenal … Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top