Mkufunzi
wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila akiwa Afisa Mtendaji Mkuu
wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama
Shekha Nasser Wakati wa Mafunzo hayo leo.
Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up". Hapa washiriki watajua namna mbalimbali za kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Mwanza na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi.Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri. Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake 65 wa Jiji la Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Mwanza wameishukuru Taasisi
ya Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mrdai huu.
Wakieleza zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata
taarifa kwa wanawake wenzao wa mkoa wa Dar es salaam kunufaika na mradi
huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo.Wakiendelea
zaidi wamesema wapo tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi
huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea kipato
Wanawake
wa jiji la Mwanza walionufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers
wakikisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa kwenye
Mafunzo hayo Yanayoendelea Jijini mwanza..
Mafunzo
ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano
yameanza mkoani Mwanza. Washiriki wa fursa hiyo wanajulikana kama
Manjano Dream Makers kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi. Mafunzo
hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake 30 wa
Jiji la Mwanza Watapatiwa elimu kuhusu biashara, namna ya kukuza na
kuendesha biashara na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani
'financial literacy'.Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma
nzuri na bora kwa wateja na jinsi ya kujiwekea akiba.






0 comments:
Post a Comment