PICHA ZA AJALI: WAFANYAKAZI WATANO WA SERIKALI WAMEFARIKI DUNIA HUKU WENGINE WANEE WAKIJERUHIWA UKO BAGAMOYO
Pichani juu ni taswira mbalimbali kutoka eneo hilo la ajali. WATU
watano wamefariki dunia huku wengine nane wakijeruhiwa, katika ajali
iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya
Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo mkoani Pwani. Waliofariki
katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango ya Uchumi,
Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40), Tunsime Duncan,
Mwanasheria wa Wilaya na Ludovick Palangya, Mchumi. Majeruhi
waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni Ibrahim Matovu,
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa, Mhandisi wa
Maji wilaya, Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri, Mweka
Hazina wa Wilaya, Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda,
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari
Mohamed, Mwananchi. Aliyepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Bagamoyo na kuruhusiwa ni George Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na
Utawala wa Wilaya. Ajali
hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yote yakitokea Bagamoyo
kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati
hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge. Magari
yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo
yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na
kuwajeruhi wengine kadhaa. Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo
lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa
lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na
kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge.
Item Reviewed: PICHA ZA AJALI: WAFANYAKAZI WATANO WA SERIKALI WAMEFARIKI DUNIA HUKU WENGINE WANEE WAKIJERUHIWA UKO BAGAMOYO
Rating: 5
Reviewed By: Unknown
0 comments:
Post a Comment