https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    TEGEMEA MABADILIKO 5 MAKUBWA EPL KAMA ITAKUWA NI KATI YA MOURINHO NA GUARDIOLA MSIMU UJAO

    Mou-Pep
    Upinzani kati ya Mourinho na Guardiola utaendelea
    Mou-Pep 1
    Wote tunajua ni kwa kiasi gani upinzani ulivyo mkubwa kati ya Barcelona na Real Madrid ulivyokua hasa katika enzi za Mourinho na Guardiola wakiwa katika utawala katika vilabu hivyo.
    Dunia nzima itakuwa tayari kushuhudia uhasimu mwingine ambao utakuwa ni wa awamu ya pili katika nchi tofauti.
    Mourinho tayari ana uzoefu na Ligi kuu ya Uingereza akiwa ameifundisha klabu ya Chelsea kwa vipindi viwili tofauti litakuwa jambo la kufurahisha kuona ni kwa kiasi gani Guardiola anaweza kufanikiwa akiwa na Man City.
    Ligi kuu ya Uingereza inachangamoto kubwa sana imeshuhudia makocha wakubwa waliofanikiwa kuja na wengi wao wameishia kuchemka na hatimaye kutimka.
    Jiji la Manchester litatawala soka Uingereza
    Mou-Pep 2
    Guardiola na Mourinho mara zote wanachukua makombe katika sehemu wanazofundisha. Kuna kila sababu wanaweza kufanya hivyo katika vilabu vikubwa vya Jiji la Manchester. Kwa usajili mkubwa wa wachezaji wa kiwango cha dunia na makocha wenye uwezo mkubwa itakuwa ni shida kwa vilabu vingine kuweza kuleta changamoto kwa klabu hizo za jiji la Manchester.
    Jiji la Manchester litakuwa jiji kubwa la Soka na litalipoteza kabisa Jiji la London ambalo ndiyo lina vilabu vingi sana pale nchini Uingereza.
    Usajili wa Gharama
    Mou-Pep 3
    Kutokana na Pep Guardiola na Jose Mourinho kujiunga na ligi ya EPL tutegemee majina makubwa pia kuja katika ligi hiyo, na ikiwa makocha wote maweshafanikiwa kufundisha wachezaji wenye majina makubwa Duniani basi litakuwa ni suala la muda tu kabla EPL haijashuhudia ujio wa mastaa katika ligi hiyo.
    Kuna kila ushawishi kwa wachezaji kuja katika ligi ya uingereza, kwanza ni ushindani wa ligi hiyo, mashabiki wenye mzuka, na mashabiki ni wengi. Lakini pia kuna pesa ya kuitosha hiyo ikithibitishwa na rekodi za usajili zinazowekwa na kuvunjwa kila mwaka.
    Pesa dhidi ya Historia
    Mou-Pep 4
    Manchester United miaka yote wanasifika kwa kuwa na Historia na utamaduni mzuri hasa linapokuja suala la soka, wakati huo kwa upande wa pili Manchester City wao wanategemea mchezaji aweze kuchagua kati ya pesa au historia.
    Kucheza Manchester United ni tofauti sana na kucheza Manchester City, Manchester City  hawawakaribii hata kidogo katika suala la makombe. Wachezaji wanachagua klabu gani na meneja gani wa kufanya naye kazi lakini ipo wazi kuwa wachezaji wengi wanatamani kucheza katika klabu ambayo ina maamilioni ya mashabiki duniani (United) na wengine wanaweza kuchagua kutengeneza historia na klabu kwa kuanza chini kabisa (City)
    Uwezekano wa kuwa na Messi na Ronaldo katika EPL
    Mou-Pep 5
    Makocha wawili bora Duniani ni wazi kuwa wanaweza kuwaajiri wachezaji wawili bora Duniani kwa sasa. Hebu fikiria kuangalia mechi ya wapinzani wa jadi kati ya Man City na Man United huku kwa upande wa City wakiwa na Lionel Messi na upande wa United wakiwa na Cristiano Ronaldo.
    Nafasi ya jambo hili kutokea ni kubwa sana ukitegemea wachezaji wote hawa wameshawahi kucheza chini ya makocha hawa wawili katika nyakati zilizopita na wanaweza kuvutiwa kufanya nao kazi tena kwa mara nyingine.

    Ronaldo ana kila sababu za kufikiria suala la kurudi United kutokana na kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 6 akifanikiwa kunyakua makombe ya kutosha lakini kikubwa zaidi mashabiki wa United wanamkubali. Ronaldo aliondoka United kwa amani japo kuwa hakuachana vizuri na Mourinho pale Estadio Santiago Bernabeu lakini kutokana na Sir Alex Ferguson kuwa katika Utawala pale Old Trafford tegemea kabisa amani kuwepo kati ya Mourinho na Ronaldo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TEGEMEA MABADILIKO 5 MAKUBWA EPL KAMA ITAKUWA NI KATI YA MOURINHO NA GUARDIOLA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top