1. Taasisi iwe katika mfumo unaoeleweka
Moja makubwa ya uzembe yaliyowahi kutokea katika historia ya usajili kwenye soka ilikuwa ni usiku wa kuamkia September 1,2015, wakati Real Madrid waliposhindwa kupata documents muhimu za kuthibitisha usajili wa David De Gea kwa sababu ya matatizo kwenye mashine yao FAX na matokeo yake uhamisho huo ukashindikana. Tukio hilo lilitoa ishara ya mambo yatakavyakuwa msimu huu.
* Mwezi December, waliondolewa kwenye michuano ya Copa del Rey kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakupaswa kucheza kisheria, Denis Cheryshev alitakiwa kutocheza mechi moja ili amalize adhabu yake ya kufungiwa.
*Mwezi January, James Rodriguez alikimbizwa na polisi kutoka kwenye uwanja wa mazoezi huko Valdebebas kutokana na kuendesha gari kwa spidi iliyokuwa ikikadiriwa kufikia 200kph.
Taswira tunayopata kutokana na matukio hayo inaonyesha kuna tatizo ndani ya klabu, na yanayojiri hayaendani na hadhi ya klabu. Madrid inahitaji kurudisha utaratibu wa kueleweka unaondena na hadhi yake. Tayari msimu huu ishathibitika kwamba ni vigumu kuikamata Barcelona dimbani, hivyo wanahitaji kuhakikisha hawaachwi mbali kwa ubora nje ya uwanja pia.
2. Kujenga Timu Vizuri
Kwa timu ambayo inashindania mataji na haiogopi kutumia fedha kufanikisha hilo kwa usajili, kuna mashimo makubwa katika kikosi cha Real Madrid kwa sasa. Inawezekanaje timu nzima kuna beki mmoja tu wa kushoto?
Marcelo ndio mchezaji pekee wa safu ya ulinzi upande wa kushoto wa kikosi cha kwanza, hivyo akiwa na majeruhi ni aidha Danilo au Dani Carvajal ambao inawabidi kucheza kwenye nafasi hiyo. Mshambuliaji wa kati, kushindwa kwa Cristiano Ronaldo kumudu kucheza vizuri kwenye nafasi hiyo kunamaanisha Karim Benzema ndio chaguo pekee la kikosi cha kwanza, hali iliyopelekea Zinedine Zidane kumpandisha Borja Mayoral kutoka kikosi cha Castilla na alicheza mechi yake kwenye mechi dhidi ya Atletico. Kwenye nafasi ya kiungo mkabaji hali nayo ni mbaya zaid: Casemiro ndio mtu pekee anayeweza kufiti kwenye nafasi hiyo, lakini bado mbrazili huyo hajaanza mchezo wowote tangu December.
Kutokuwa na wachezaji mbadala kwenye maeneo hayo matatu muhimu ni jambo ambalo linawagharimu na halina utetezi kutokana na rasilimali walizonazo Madrid, jambo ambalo linapelekea kocha kuwa na kazi ngumu kuunda timu ambayo itakuwa ina balance. Hilo haliwezi kuendelea.
3. Cristiano Ronaldo Auzwe
Kama mfungaji wao bora wa muda wote, nafasi ya Ronaldo katika historia ya Real Madrid tayari haina mpinzani, lakini haina ubishi kwamba ni vigumu kuendelea kumhukumu Ronaldo kutokana na yale aliyoyafanya nyuma, na kiuhalisia kwasasa nahodha huyo wa Ureno yupo kwenye anguko la kiwango chake.
Takwimu za mshambuliaji huyo bado zinaonekana vizuri kwenye karatasi lakini zinaweza kuwa zinaongopa: Magoli 22 aliyofunga kwenye msimu huu wa 2015/16 katika ligi mpaka kufikia mwisho wa mwezi uliopita, asimia 70 kati ya hayo yametokana na timu ambazo zipo kwenye nusu ya timu za mwisho kwenye msimamo wa ligi. Unganisha hilo na la kushindwa mpaka sasa kuzifunga Barcelona, Atletico Madrid, Villarreal na Sevilla msimu huu, utaanza kupata jibu halisi la muelekeo wake.
Wakati Ronaldo ambao hafungi magoli huwa ana kawaida ya kuwa kikwazo cha kiufundi kuliko suluhisho, na hilo huwa tatizo zaidi kwenye mechi kubwa. Hushikwa na hasira na kufanya vitendo ambavyo huhatarisha kupata kadi nyekundu, na kufanya mambo kuwa magumu zaidi ameanza tabia ya kuwasema wachezaji wenzake kwa viwango kwenye vyombo vya habari.
Suluhisho ni kumuuza, Madrid wanahitaji kujenga upya timu yao, na Ronaldo akiendelea kuwepo hawawezi kutimiza lengo hilo. Timu iliyo na balanced zaidi, isiyokuwa na focus ya kuangalia wachezaji binafsi zaidi – Real Madrid ya namna hii itakuwa na uwezo wa kushindana zaidi na kuwasababisha Barca matatizo zaidi.
4. Kuwa na plan inayoeleweka na utambulisho sahihi
Matatizo ya Madrid katika miaka ya hivi karibuni yanaweza kupata suluhisho kwa kuangalia mfano mmoja tu wa mahasimu wao wa jiji la Madrid. Kabla ya kuwasili kwa Diego Simeone, Atletico walikuwa wamecheza mechi 22 bila kushinda mechi dhidi ya Madrid, lakini tangu Simeone aliposhika madaraka ya ukocha wamefanikiwa kushinda 7 dhidi ya Los Blancos, zikiwemo mechi 6 mfululizo za ligi ambazo wamecheza bila kufungwa. Simeone ameiwezesha Madrid kushinda mechi 3 mfululizo pale Santiago Bernabeu, kitu ambacho hakuna timu kwenye La Liga imewahi kufanya kwenye historia ya michuano hiyo.
Ukiangalia uwezo wa kiuchumi walionao Madrid, hakuna namna ambayo wangeshindwa kupata ushindi kila mara dhidi ya wapinzani wao, sasa ni namna gani Atletico wameweza kujijenga na kuweza kuimudu Madrid pamoja na kuondokewa na wachezaji wao muhimu kila msimu. Hakuna siri nyingine zaidi ya style ya uchezaji inayoeleweka ya Atletico: Wanaweka safu ngumu ya ulinzi, wanacheza counter attacks, na sasa wanaimarisha uwezo wao katika kumiliki mpira. Wanaposajili wachezaji siku zote husajili wachezaji ambao wanaweza kufiti kwenye mfumo wao. Style ya Real Madrid hata haieleweki.
Real Madrid walitoka kwenye mchezo wa kuvutia na pasi fupi fupi za mfumo wa Manuel Pellegrini, mpaka kwenye mfumo wa counter-attacking chini ya Jose Mourinho, wakapita kwenye mfumo tofauti wa Carlo Ancelotti. Wakaingia kwenye mfumo wa kukaba sana chini ya Rafa Benitez, na sasa wapo kwenye mfumo tofauti wa kumiliki mpira chini ya Zinedine Zidane. Kila anapoondoka kocha mmoja mfumo unabadilika na timu inaanza moja ku-adapt mfumo wa kocha mwingine.
Kutokana na tatizo hilo la kukosa mfumo unaoeleweka, ni jambo ambalo halishangazi kuona Madrid wakiwa wanacheza kama kuku asiye na kichwa. Klabu inahitaji sana kuwa na mfumo unaoeleweka. Ikiwa wanahitaji mifano halisi waangalie wapinzani wao wa pembeni mwa jiji lao, au Barcelona ambao wana staili moja ya uchezaji hata baada ya mabadiliko ya makocha kadhaa kwa muongo uliopita.
5. Raisi Anayeingilia kila kitu nae Aondoke
Hakuna mabadiliko yanayoweza kufanyika pale Snatiago Bernabeu bila kumuondoa kiongozi mkuu. Florentino Perez huwa anajiona yeye ni kocha wa mpira, lakini matokeo yanaonyesha ni mmoja wa makocha wabovu kabisa.
Madrid wamefanikiwa kushinda ubingwa mara moja tu ndani ya miaka 7 chini ya uongozi wa Perez – ukame wa makombe umetokea wakati wa utawala wa Raisi huyu anayeingilia kila kitu, ambaye anatajwa kuwa na tabia za viongozi wa Simba na Yanga za kuingilia mpaka upangaji wa kikosi na amekuwa na mamlaka kwenye kuamua nani wa kusajiliwa na nani wa kutokusajiliwa na nani wa kufukuzwa na nani abaki.
Hatimaye, mashabiki wa Real Madrid wameanza kuamka – kwa mara kadhaa msimu huu mashabiki wamekuwa wakiimba nyimbo za kumtaka Perez ajiuzulu.
Kumpata mrithi wake haitakuwa rahisi kutokana na mfumo thibiti uliowekwa na Perez wa kupata mgombea miongoni mwa wajumbe 88 katika wananchi 46 million waliopo Spain, ni vigumu kuamini kwamba hata miongoni mwa namba hiyo ndogo hakuna mtu wa kumudu kufanya kazi nzuri zaidi ya Raisi aliyepo.
Kumfukuza Perez sio kitu kitakacholeta mabadiliko ya haraka, na haiwezi kuifanya Madrid iweze kushindana na Barcelona, lakini mabadiliko kwenye uongozi wa juu yataruhusu Madrid kuendelea mbele.
0 comments:
Post a Comment