Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta bado hajakuwa
na wakati mgumu na Timu yake ya KRC GENK inayoshiriki ligi kuu Ubeligiji
Pro League kama wanavyodhani watu wengi. Samatta anatokea benchi kwenye
mechi zote alizocheza hadi sasa kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa
ugiriki Karelis Nikolous.
Kuonesha kwamba yupo vizuri, wikiendi iliyopita Samatta alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza klabuni hapo walipokutana na vinara wa ligi hiyo Club Brugge. Makala hii inakuletea takwimu muhimu kuhusu Mbwana Samatta, jezi namba 77 dhidi ya Mgiriki Karelis Nikolaos namba 7 ambaye mara kadhaa anapotoka Samatta anaingia
Magoli (1 vs 4)
Mbwana Samatta hadi sasa amefanikiwa kupachika wavuni goli 1, wakati Mgiriki Nikolous amefunga mara 4. Samatta alifunga goli lake kwenye mchezo dhidi ya Club Brugge dakika 81 baada ya kutokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Karelis Nikolous.
Mechi (4 vs 7)
Mbwana amecheza michezo mine (4) akiwa na KRC GENK, ambapo Karelis amecheza mechi saba (7) hadi sasa ndani ya msimu huu 2015/2016.
Dakika (71 vs 429)
Hizo ndizo dakika ambazo wakali hao wametumia dimbani. Kwenye mechi nne ambazo samatta amecheza ametumia dakika 71 wakati Nikolous ametumia dakika 429.
Kutokea benchi (4 vs 1)
Kwenye michezo yote minne ambayo Mbwana Samatta amecheza klabuni hapo, amekuwa akiingia kutokea benchi. Kwenye mechi zote nne aliingia kuchukua nafasi ya Karelis Nikalaos. Karelis ameanzia benchi mechi moja tu.
Kadi za njano (1 vs 0)
Mbwana samatta amepata kadi moja tu ya njano hadi sasa kwenye michezo minne aliyocheza. Kadi ambayo ameipata kwenye mechi dhidi ya Brugge wakati Karelis hana kadi yeyote.

0 comments:
Post a Comment