https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    UCHAMBUZI :Real Madrid 1-1 Atletico Madrid (AET, 5-3 penati)

    Real Madrid parade European Cup on open-top bus tour after returning home from Milan as
     Na: Chikoti Cico
    1. Real Madrid sio tu kwamba wana uhusiano mzuri na michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya bali pia wanajua namna ya kucheza fainali za michuano hii na kushinda, mara 14 ameingia fainali za Champions League/European Cup na kunyakua kombe hilo mara 11 (A por la decima)
    2. Wanaume 22 wamekimbiza mpira kwa dakika 120 ila mwishowe Cristiano Ronaldo ndiye aliyevua jezi kushangilia, hakuwa asilimia 100 leo, muda mwingi alikuwa mtembezi lakini wenyewe wanamwita "THE MAN OF THE MOMENT" muda wake ulifika naye akafanya IPASAVYO. Ballon d'or imerejea ilipotoka.
    3. Hiki alichokifanya Zidane kinaitwa "Football is a simple game" mshikaji amepewa kazi ndani ya miezi mitano na akafanya kile ambacho makocha lukuki duniani hawajawahi kukifanya ndani ya muda huo, hakika "soka ni mchezo mrahisi". 1998 alifanya akiwa na jezi ya Madrid, leo amefanya tena akiwa na suti. Zidane historia yake pale Bernabeu itaandikwa kwa kalamu ya dhahabu.
    4. Kama utatu mtiifu wa BBC ni wachezaji bora wa Real Madrid basi LUKA MODRIC ni mchezaji MUHIMU wa klabu hiyo, achana na zile pasi za nje ya kiatu (visu), huyu ndiye aliyeamua Real wacheze vipi, wakati gani washambulie na wakati gani wazuie.
    5. Kama Diego Simeone ni mhuni ambaye mtaani/ uswahilini kote wanamjua basi Zidane ni mhuni mitaa ya kota/ wakishua, leo Zizou amecheza KIATLETICO na kuondoka na kombe, kwanza kabisa aliwapa mipira yote AM na kuamua kushambulia kwa "counter attack" ambayo imemlipa sana. RM wangecheza mfumo wao wa kawaida leo wangeangukia pua, walijaribu mara 10 dhidi ya AM wakafanikiwa mara moja tu.
    6. Diego Simeone, utakumbukwa kwa kujua kuingia fainali za UCL mara mbili tena kwa kuwaondosha vigogo ila nachelea kusema bado hujajua namna ya kucheza fainali hizi kubwa ama namna ya kucheza na Real Madrid fainali. Leo umeshindwa kwasababu umeshindwa.
    7. Atletico Madrid ni klabu ambayo imejengwa kwa mfumo wa kukaba kwa karibu wakati wote wa mchezo ila kitendo cha leo RM kuwapa nafasi ya kumiliki mpira kwa muda mrefu kilifanya hatari ya AM ipungue sana kwasababu sio mfumo wao na hatimaye RM ndiyo wakaonekana kuwa na hatari zaidi pamoja na kwamba mipira mingi ilikuwa kwa AM.
    8. Saul na Carrasco, hawa wachezaji wawili vijana wakiendelea na kasi hii basi klabu kubwa Ulaya, pesa nyingi zitawatoka, ni viungo mahiri sana kuanzia kwenye ukabaji mpaka kushambulia, kuhusu Carrasco nafikiri Danilo hatamsahau baada ya usiku wa leo.
    9. Nyuma ya Juanfran, Savic, Godin na Filipe Luis kulikuwa na MTU mahiri jinale JAN OBLAK, kama sio kijana huyu mwenye miaka 23 basi hali ingekuwa mbaya zaidi kwa AM, alikuwepo De Gea halafu Courtois na sasa Oblak, naona dunia ya soka imepata soko la makipa liitwalo "ATLETICO MADRID".
    10. TAKWIMU: Sergio Ramos ni mlinzi wa kwanza kufunga ktk fainali mbili za ucl, Zinedine Zidane ni Mwanadamu wa pili ndani ya Madrid kunyakua UCL/ European Cup kama mchezaji na kama kocha, mwingine ni Miguel Muñoz, Toni Kroos ni mchezaji wa 13 kunyakua kombe la UCL na klabu mbili tofauti.
    NB: Real Madrid wamezifunga timu lukuki leo ikiwemo Barcelona na wengineo wengi waliojificha nyuma ya Atletico Madrid.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCHAMBUZI :Real Madrid 1-1 Atletico Madrid (AET, 5-3 penati) Rating: 5 Reviewed By: Anonymous
    Scroll to Top