Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara na namna ya kuendesha Ujasiriamali Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma .
Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika fursa hiyo na wanajulikana kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake hao kutoka Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa za ujasiriamali, changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa pamoja na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na kujua mbinu zipi watumie kujiwekea akiba.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo ya Ujasirimali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma..
Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up Artistry". Awamu hii hapa washiriki watajua matumizi yenye ueledi (professional) wa kutunza ngozi, kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Dodoma na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi sahihi na salama. Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri katika tasnia ya vipodozi.
Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi Pendwa vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake Zaidi ya 150 Kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Visiwani Zanzibar. Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Dodoma wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mradi huo.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa Dododma.
Wakieleza zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa wanawake wenzao wa mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar kunufaika na mradi huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo. Wakiendelea zaidi wamesema wapo tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea kipato kupitia kazi ya mikono yao
0 comments:
Post a Comment