Kampeni chafu dhidi ya Neymar zimerejea tena, safari hii hazitokei Madrid, bali upande wa Barcelona wenyewe.
Wakati
timu ikiwa inahitaji msaada kutoka kila mmoja anayeizunguka klabu, ili
kuondokana na matokeo mabaya ya hivi karibuni, vyanzo viwili vya vyombo
vya habari vimeanzisha kusambaza taarifa kwamba maisha halisi ya Neymar
yanaathiri kiwango chake dimbani, na inataarifisa kwamba vyanzo hivyo
vya habari vinafanya yote vikiwa na sapoti kutoka kwa baadhi wajumbe ya
wakurugenzi ya Barca.
Vyanzo hivyo habari vimetoa taarifa kwamba tabia ya Neymar kupenda kula sana bata, kusafiri bila ushari mzuri wa kitabibu, kwenda kufanya matangazo binafsi ya biashara, na mambo mengine kumepelekea kuathirika kwa kiwango chake. Vyanzo hivyo vya habari vinasema kwamba kumekuwepo na malalamiko kutoka ndani ya klabu kutokana na tabia hizo za nahodha huyo wa Brazil.
Taarifa za vyanzo hivi vya habari zinaonekana kutolewa na sehemu ya bodi ya wakurugenzi ambao wamekuwa wakikerwa na kiwango cha Neymar. Baadhi ya wajumbe hao pia wamekuwa wakishauri wenzao mshambuliaji huyo auzwe mwishoni mwa msimu kwa ada ya 190 million ambayo imetajwa kwenye mkataba katika kipengele cha kuvunja mkataba.
Gazeti
la Sport ambalo maskani yake ni Catalunya limeripoti taarifa hii na
kusisitiza kwamba taarifa hizi zimekuja wakati kukiwa na tetesi juu ya
Madrid kuendelea kummezea mate Neymar huku habari kutoka England
zikisema Manchester United wapo tayari kulipa kiasicha £150m kupata
saini ya Neymar.
Vyanzo hivyo habari vimetoa taarifa kwamba tabia ya Neymar kupenda kula sana bata, kusafiri bila ushari mzuri wa kitabibu, kwenda kufanya matangazo binafsi ya biashara, na mambo mengine kumepelekea kuathirika kwa kiwango chake. Vyanzo hivyo vya habari vinasema kwamba kumekuwepo na malalamiko kutoka ndani ya klabu kutokana na tabia hizo za nahodha huyo wa Brazil.
Taarifa za vyanzo hivi vya habari zinaonekana kutolewa na sehemu ya bodi ya wakurugenzi ambao wamekuwa wakikerwa na kiwango cha Neymar. Baadhi ya wajumbe hao pia wamekuwa wakishauri wenzao mshambuliaji huyo auzwe mwishoni mwa msimu kwa ada ya 190 million ambayo imetajwa kwenye mkataba katika kipengele cha kuvunja mkataba.

0 comments:
Post a Comment