https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Besigye ashtakiwa kwa kuingia Kampala

    Image captionKiiza Besigye na wafuasi wake
    Polisi nchini Uganda wamemfungulia mashtaka kiongozi wa upinzani daktari Kiiza Besigye kwa kujaribu kuingia jijini Kampala kwa msafara wa magari
    Msemaji wa polisi anasema kuwa kiongozi huyo wa upinzani alikaidi amri ya kutoingia mjini Kampala kufuatia maelfu ya mashabiki wake kuzingira gari lake huku wengine wengi wakimfuata na kuunda msafara wa magari.
    Image captionUganda yamfungulia Besigye mashtaka
    Polisi wanasema kuwa Besigye alikuwa amepewa idhini ya kuhudhuria hafla ya maombi katika makao makuu ya chama chake ilimradi tu asivuruge amani na utangamano mjini Kampala.
    Hata hivyo polisi walimzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya karibu sana kuingia mjini.
    Image captionpolisi walimzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya
    Mwandishi wa BBC aliyeko Kampala Patience Atuhaire anasema polisi wamezuia watu kufuata gari la kiongozi huyo wa chama cha FDC.
    Polisi wametumwa kwa wingi eneo hilo.
    Gari la Bw Besigye lilibururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
    Image captionGari la Bw Besigye lilibururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
    Bw Besigye ambaye amekuwa katika kifungo cha nyumbani alikuwa ndio anatoka nyumbani kwake kwa mara ya kwanza hii leo tangu uchaguzi kufanyika nchini Uganda.
    Kiongozi huyo wa upinzani alimaliza katika nafasi ya pili lakini akapinga matokeo hayo ya uchaguzi akisema kuwa rais Museveni alikuwa amefaidika na udanganyifu mwingi na kuwa uchaguzi huo haukuwa wa uhuru wala haki.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Besigye ashtakiwa kwa kuingia Kampala Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top