Mwongozo wa vyoo 100 bora zaidi duniani umechapishwa na kampuni ya usafiri ya Lonely Planet.
Mwongozo huo umeorodhesha vyoo vya kila aina ambavyo bila shaka vina uwezo wa kuwaacha wasafiri vinywa wazi au kuwa na kumbukumbu za kusalia nazo daima.
“Vyoo ni dirisha la kuingia ndani katika moyo wa pahala Fulani. Isitoshe, bila kujali unavipa jina gani, vyoo huwaweka watu wote katika ngazi sawa,” kitabu hicho kinasema.
Hapa chini ni baadhi ya vyoo vilivyo kwenye mwongozo huo.
Vyoo hivi vinapatikana Chott, Tunisia katika ziwa la maji ya chumvi lililokauka. Hapa ndipo video ya nyumba ya Luke Skywalker katika filamu ya Star Wars ilichukuliwa.
Vyoo hivi katika eneo la Bahia, Brazil vimo katika kituo cha kutunza kasa.
Choo hiki ambacho kinapatikana eneo lenye mandhari ya kupendeza kinapatikana Uswizi. Hapa ni mita 2,7000 katika milima ya Alps.
Choo hiki katika duka la Standard Grill katika mtaa maarufu wa kufungia nyama New York kimeelezwa na wengi kama choo kinachokanganya ubongo.
Vyoo hivi vijulikanavyo kama Between The Waters vinapatikana Emscherkunst nchini Ujerumani.
Hapa ni Wellington, New Zealand. Kwa kutazama picha, ni vigumu kuelewa vyoo hivi hutumiwa vipi. Lakini waliozijenga walitaka zifanane na miguu ya kambakoche.
0 comments:
Post a Comment