MWAKA unaelekea ukingoni, kuna mengi yametokea ndani ya mwaka huu wa 2015 katika jamii yakiwemo mazuri na mabaya.
Kama
ilivyo kawaida katika ulimwengu wa mastaa hakukosekani vituko vya hapa
na pale, leo katika makala haya tunakuletea mastaa mbalimbali
waliotikisa kwa skendo za mapenzi, yaani waliokuwa na misuguano na
wengine kutajwa kubadili wapenzi kila kukicha.
DIAMOND NA ZARI
Staa
huyu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenziye Zarinah
Hassan ‘Zari,’ walitikisa mwaka huu kwa kupamba vyombo mbalimbali vya
habari hasa pale walipopata mtoto Tiffah ambaye ilisemekana siyo mtoto
wa msanii huyo na kutajwa kuwa ni wa mume wa zamani wa Zari, Ivan
Semwanga na wengine wakidai ni wa pedeshee Muzamil Katunzi, skendo hii
ilitikisa lakini Diamond akashikilia msimamo wake kwamba mtoto ni wa
kwake.
Wawili
hao pia walidaiwa kwamba baada ya kupata mtoto mkataba ulikwisha na
sasa Zari anaishi kwake huko Afrika Kusini, hii ilitokana na kushindwa
kuishi na mama Diamond kwani alidai familia hiyo ina mambo ya Kiswahili
ambayo hakuweza kuyakabili.
NAY NA SHAMSA
Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Shamsa
Ford ambaye ni msanii wa filamu ishu yao ya kuwa wapenzi ilitikisa sana
ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Nay kuachana na mzazi mwenzake, Siwema
Edson ambapo ilisemekana mapenzi yake na Shamsa yalikuwepo hata kabla
hajaachana na mwanamama huyo.
Nay
hakuishia hapo, baada ya kutajwa kuwa kwenye uhusiano na Shamsa pia
alinaswa na msanii wa Bongo Fleva, Pam D wakiwa kwenye pozi tata la
kimapenzi na baada ya hapo hivi karibuni akahamia kwa mrembo kutoka
Marekani, Stella Tilya ‘Chaga Baby’.
WEMA SEPETU NA LUIS MNANA
Mrembo
huyu asiyeishiwa matukio, mwaka huu aliingia kwenye vichwa vya habari
kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mshiriki wa Big Brother Africa
(BBA)ambaye ni raia wa Namibia, Luis Mnana na kufanikiwa kumbadilisha
dini na kuwa Muislamu ili waweze kufunga ndoa.
Kwa bahati mbaya wawili hao hawakuweza kufikia kufunga ndoa, waliachana na sasa kila mmoja yupo na maisha yake.
JOKATE NA ALI KIBA
Wawili hawa wamesumbua sana mwaka huu kwani ni wapenzi ambao walikuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali za starehe.
Penzi
hili limekuwa na misukosuko kwani wazazi wa Jokate hawapendi awe na Ali
Kiba hata wale wa upande mwingine hawampendi mwanadada huyo.
LULU NA CHENI
Wasanii
hawa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’
walitikisa na skendo ya kutaka kuoana ambapo kila mmoja alifunguka lake.
Wawili hao mpaka sasa haijulikani kinachoendelea kuhusu ndoa licha ya Mama Lulu kukubali mwanaye aolewe Kiislamu.
AGNES MASOGANGE NA DAVIDO
Mwanadada
huyu ambaye ameonekana kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo
Fleva, mwaka huu alitikisa na skendo ya kutoka kimapenzi na Mwanamuziki
wa Nigeria, Davido.
Pamoja
na kuwa na msanii huyo pia alikumbwa na skendo ya kuvunja amri ya sita
na wanaume wawili kwa wakati tofauti kwenye hoteli moja ya Ramada, Dar.
CHANZO;GPL


0 comments:
Post a Comment