Kitendo
cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry
Kitilya pamoja na maofisa wawili waandamizi wa zamani wa Benki ya
Stanbic, Tawi la Tanzania, Sioi Solomoni na Shose Sinare kubeba ndoo
wakati wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuelekea mahabusu,
kimezua maswali mengi.
Kitilya
na wenzake hao walifikishwa kwenye mahakama hiyo na kusomewa makosa
manane likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za
Marekani.
Sinare
aliyekuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, anakabiliwa na mashtaka
mengine mawili ya kughushi na mengine ya kuwasilisha nyaraka za uongo za
Serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Marekani 550 milioni kutoka
Benki ya Standard ya Uingereza kati ya mwaka 2012 na 2013.
Mvutano
wa kisheria ulioibuka mahakamani hapo juzi ulimfanya Hakimu Elimius
Mchauru anayesikiliza kesi hiyo kuamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu
hadi Aprili 8, mwaka huu atakapotoa uamuzi kama watuhumiwa hao wana haki
ya kupewa dhamana au la.
Wakati
wakiondoka kwenda kupanda magari tayari kwa kuelekea gerezani,
washtakiwa hao walikuwa wamebeba ndoo ndogo za plastiki. Kitilya
alionekana akiwa amebeba ndoo moja, Sioi mbili na Sinare moja.
Ndoo
hizo zimezua maswali mengi bila majibu ikiwamo sababu ya kuzibeba, muda
uliotumika kuziandaa au kama walikwenda nazo mahakamani wakijua
watakosa dhamana na kupelekwa mahabusu.
Pia, maswali yameibuka kuwa walikuwa wakienda nazo mahabusu kufanya nini na je, mahabusi wote huenda na ndoo? Au ni wao tu.
Wakili
wa kujitegemea wa kampuni ya uwakili ya Kakamba and Partiners, Mathew
Kakamba alisema ameshangaa kuona watuhumiwa wanaelekea mahabusu wakiwa
na ndoo.
Alisema hakuna sheria inayoruhusu mtuhumiwa yeyote kwenda na kitu chochote huko na ndiyo maana hufanyiwa upekuzi.
“Ndiyo
maana hata mkanda, simu na vifaa vingine wanatakiwa kuviacha mapokezi,
sasa sijajua kama hizo ndoo waliruhusiwa kuingia nazo au la,” alisema.
Akizungumzia
suala hilo, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje alisema
huenda walikuwa wamehifadhia baadhi ya vitu vyao ambavyo wangekwenda
navyo mahabusu.
“Labda
wamebeba kwa ajili ya kuogea au kuhifadhia baadhi ya vitu vyao lakini
kwa Magereza za Dar es Salaam hakuna tatizo la maji,” alisema Mboje.
0 comments:
Post a Comment