Mafundi wa kampuni ya Estim Construction wakiendelea na Ujenzi wa barabara ya Mwenge –Morocco KM 4.3 ambayo ni sehemu ya Barabara ya
Morocco –Mwenge-Tegeta.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS akimuonyesha Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng.Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge KM 4.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Watatu kushoto) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (Hawapo pichani) huku Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Agness Kijazi ( Watatu kulia) akifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dkt Agness Kijazi akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano moja ya ramani zinazotumika katika masuala ya utabili wa hali ya hewa.
Mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa nchini Didasian Kankesha akifuatilia utabiri kabla ya uhakiki na kuutangaza kwa wadau.
Mtaalam wa kusoma utabiri wa hali ya hewa Hellen Msemo akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano namna taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinavyorekodiwa na kutumwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa TMA kuhusu namna ya kufanya kazi kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma ramani ya utabiri wa hali ya hewa katika chumba maalum
cha kusoma ramani mara baada ya kukagua ofisi za Mamlaka ya hali ya hewa
nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa mkandarasi ESTIM Construction anayejenga barabara ya Bagamoyo, Sehemu ya Morroco-Mwenge kilomita 4.3 kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema baada ya wiki mbili barabara hiyo itafunguliwa kwa ajili ya matumizi ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katikati ya jijini.
“Hakikisheni barabara hii inakamilika ndani ya wiki mbili, ili msongamano wa magari yanatoingia na kutoka katika ya jiji upungue, na hivyo kuiunganisha vizuri barabara hii na ile ya Mwenge-Tegeta”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha amewataka waananchi na madereva wanaotumia barabara hiyo kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vya kumwaga mafuta kwenye barabara hiyo na kutupa takataka zinazosababisha mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuzipa na kuharibu barabara hiyo.
“Nawataka watumiaji wa barabara, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara, tunawekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara mijini ili kuondoa msongamano hivyo zingatieni matumizi sahihi ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu”. Amesema Prof. Mbarawa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwa ili kupunguza msongamano ujenzi wa barabara hiyo umelazimika kuweka sehemu maalum za watembea kwa miguu kutokana na wingi wa watumiaji wa barabara hiyo katika sehemu hiyo na kupanua maingilio ya barabara ili kurahisisha magari kutoka na kuingia katika barabara hiyo.
Eng. Mfugale amesema zaidi ya magari 15,000 yanakadiriwa kuwa yatapita katika barabara itakapokamilikana hivyo kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo katika eneo hilo.
Takribani shilingi bilioni 4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo na hivyo
kuiunganisha barabara ya Mwenge-Morroco na ile ya Mwenge-Tegeta.
Amesema iwapo Mamlaka hiyo itafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu itaongeza idadi ya watu inaowahudumia kwa mwaka nchini na hivyo kusaidia wadau mbalimbali wa sekta za Kilimo, Ujenzi, Afya, Uvuvi kufanya kazi kwa faida.
Prof. Mbarawa amekagua vitengo cha takwimu za hali ya hewa, hali ya hewa ya kilimo na Utabiri na kusisitiza kuwa ni wakati wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati mmoja.
“Hakikisheni taarifa zenu zinawafikia watu wengi hususanwale wanaozihitaji taarifa hizi kwa kutekeleza shughuli zao kiuchumi”. Amesema Prof. Mbarawa.
Naye Mkurungenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka hiyo inafanya utabiri kwa usahihi wa asilimia 80 na ni miongoni mwa Mamlaka inayofanya vizuri katika huduma za utabiri barani Afrika.
“Taarifa zetu ni sahihi na kila baada ya dakika 15 tunatoa taarifa zinazoonyesha hali ya hewa nchini”.Amesema Dkt. Kijazi.
Dkt. Kijazi amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uelewa wa watumiaji wa hali ya hewa hapa nchini ili kuwezesha wadau wa hali ya hewa kunufaika kikamilifu na utabiri unaotolewa na Mamlaka hiyo.
Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Morocco –Mwenge-Tegeta.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS akimuonyesha Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kazi ya ujenzi wa mifereji pembezoni mwa Barabara ya Morocco-Mwenge inavyoendelea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng.Patric Mfugale kuhusu kukamilika kwa upanuzi wa barabara ya Morocco-Mwenge KM 4.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Watatu kushoto) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (Hawapo pichani) huku Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Agness Kijazi ( Watatu kulia) akifuatilia kwa makini.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dkt Agness Kijazi akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano moja ya ramani zinazotumika katika masuala ya utabili wa hali ya hewa.
Mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa nchini Didasian Kankesha akifuatilia utabiri kabla ya uhakiki na kuutangaza kwa wadau.
Mtaalam wa kusoma utabiri wa hali ya hewa Hellen Msemo akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano namna taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinavyorekodiwa na kutumwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma ramani ya utabiri wa hali ya hewa katika chumba maalum
cha kusoma ramani mara baada ya kukagua ofisi za Mamlaka ya hali ya hewa
nchini.
Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo, Prof. Mbarawa amesema baada ya wiki mbili barabara hiyo itafunguliwa kwa ajili ya matumizi ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katikati ya jijini.
“Hakikisheni barabara hii inakamilika ndani ya wiki mbili, ili msongamano wa magari yanatoingia na kutoka katika ya jiji upungue, na hivyo kuiunganisha vizuri barabara hii na ile ya Mwenge-Tegeta”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha amewataka waananchi na madereva wanaotumia barabara hiyo kulinda mazingira kwa kuepuka vitendo vya kumwaga mafuta kwenye barabara hiyo na kutupa takataka zinazosababisha mifereji iliyo pembezoni mwa barabara kuzipa na kuharibu barabara hiyo.
“Nawataka watumiaji wa barabara, kuzingatia matumizi sahihi ya barabara, tunawekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara mijini ili kuondoa msongamano hivyo zingatieni matumizi sahihi ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu”. Amesema Prof. Mbarawa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwa ili kupunguza msongamano ujenzi wa barabara hiyo umelazimika kuweka sehemu maalum za watembea kwa miguu kutokana na wingi wa watumiaji wa barabara hiyo katika sehemu hiyo na kupanua maingilio ya barabara ili kurahisisha magari kutoka na kuingia katika barabara hiyo.
Eng. Mfugale amesema zaidi ya magari 15,000 yanakadiriwa kuwa yatapita katika barabara itakapokamilikana hivyo kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo katika eneo hilo.
Takribani shilingi bilioni 4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo na hivyo
kuiunganisha barabara ya Mwenge-Morroco na ile ya Mwenge-Tegeta.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA),kufanya tafiti na kuangalia fursa zitakazoiwezesha kupata mapato kutokana na kazi inazozifanya.
Amesema iwapo Mamlaka hiyo itafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu itaongeza idadi ya watu inaowahudumia kwa mwaka nchini na hivyo kusaidia wadau mbalimbali wa sekta za Kilimo, Ujenzi, Afya, Uvuvi kufanya kazi kwa faida.
Prof. Mbarawa amekagua vitengo cha takwimu za hali ya hewa, hali ya hewa ya kilimo na Utabiri na kusisitiza kuwa ni wakati wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati mmoja.
“Hakikisheni taarifa zenu zinawafikia watu wengi hususanwale wanaozihitaji taarifa hizi kwa kutekeleza shughuli zao kiuchumi”. Amesema Prof. Mbarawa.
Naye Mkurungenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka hiyo inafanya utabiri kwa usahihi wa asilimia 80 na ni miongoni mwa Mamlaka inayofanya vizuri katika huduma za utabiri barani Afrika.
“Taarifa zetu ni sahihi na kila baada ya dakika 15 tunatoa taarifa zinazoonyesha hali ya hewa nchini”.Amesema Dkt. Kijazi.
Dkt. Kijazi amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uelewa wa watumiaji wa hali ya hewa hapa nchini ili kuwezesha wadau wa hali ya hewa kunufaika kikamilifu na utabiri unaotolewa na Mamlaka hiyo.
Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

0 comments:
Post a Comment