Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo, wakiandika katika jarida la kimatibabu la Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene.
Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu.
Wanasayansi hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya kuendeshea baiskeli.
Wanazihimiza serikali kuchukua hatua za pamoja, hasa kuhusu bei ya vyakula.
Walitumia takwimu kutoka nchi 180.
0 comments:
Post a Comment