Kama
umekua nje ya Jiji la Dar es Salaam kwa muda mrefu, ni wazi kwamba ukija
utahitaji kupata maelekezo ya mambo kadha wa kadha ili kurahisisha
maisha na shughuli zako kwani kuna mabadiliko ya vitu vingi.
Pamoja
na badiliko kubwa la UTUMBUAJI MAJIPU ambalo liko kinywani mwa kila mtu
unayekutana naye, kuna mabadiliko ya matumizi ya barabara hasa zile
ambazo zinatarajiwa kutumika kwa mabasi yaliyolenga kuboresha usafiri wa
umma. Barabara hizi (hasa Morogoro na Kawawa) zimekua safi zaidi;
zimekua nyembamba ukilinganisha na awali; zimeongezwa taa za kuongoza
magari; na zina alama mpya/za ziada.
Kama
vile haitoshi, maboresho ya barabara hizi yamebadili mwelekeo wa baadhi
ya safari kwani kuna maeneo huruhusiwi tena kukata kulia au kushoto;
kuna maeneo huwezi kuingi kwenye barabara za pembeni; na kwingine
unalazimika kuchepuka na kupita njia za pembeni ili kupata barabara kuu.
![]() |
Pamoja
na maboresho haya ambayo ni wazi kwamba ni hatua moja mbele katika
upanuaji na uboreshaji wa barabara zetu kuwa za kisasa zaidi, bado kuna
tatitizo la msingi katika matumizi ya alama za barabarani kwa lengo la
kumsaidia mtumiaji. Kwa uchambuzi wangu wa haraka baada ya kupita kwenye
barabara hizi, nimeona shida kadhaa:
1. Alama
za barabarani zilizowekwa pamoja na maandishi yanayoendana nazo, ni
ndogo sana. Pamoja na ukweli kwamba barabara zetu zimepakana na
“mbwembwe” za kila aina, inahitahi umakini mkubwa kuziona na kuzielewa.
2. Alama
nyingi za barabarani zimewekwa karibu sana na mahali ambapo
zinahitajika na hivyo kumpa dereva muda mfupi sana wa kuzitafakari na
kuzielewa kabla ya kuchukua hatua
3. Alama
nyingi za muhim zimewekwa mara moja tu. Kwa mfano, unapokaribua
makutano ya Morogoro na Kawawa, kuna mbadiliko ya jinsi ya kupita kwa
wanaoelekea barabara ya Kawawa kutoka Morogoro na kinyume chake. Hata
hivyo, alama inayokupa maelekezo ya kupita (kama nimeona vizuri) iko
moja tu kuanzia huko unakotoka na iko karibu kabisa na mahali pa
kuchukua maamuzi
4. Alama
za barabarani zimewekwa kwenye vibao tu na hakuna maandishi yoyote
yaliyoandikwa chini (kwenye njia) kumsaidia dereva kuelewa zaidi na
kuepuka makosa
Iwapo
barabara hizi zitawekwa alama zote muhim kwa ukubwa, nafasi, na ubora
unaotakikana, itarahisisha sana usalama wa watumaiji na kuzuia makosa
yasiyo ya lazima kwa madereva. Pia zitasaidia kutotumika nguvu kubwa
kuwinda wakosaji na badala yake muda wa askari utatumika kwa kazi
nyingine muhim za ulinzi na usalama wa raia. Alama hizi zinapokuwa wazi
na za kutosha, zinasaidia kuiweka sawa saikolojia ya madereva na
kujikuta wanalazimika kufuata sheria na kanuni bila shuruti.
NB: Maoni
haya ni mtazamo wangu kwa kile nilichojionea kwenye barabara hizi.
Inawezekana kuna ambavyo sijaona na hivyo kutokua sahihi kwa 100% katika
yale niliyoshauri.
Mtumiaji wa Barabara.
Mwalimu MM (mmmwalimu@gmail.com
|






0 comments:
Post a Comment