1. Wameshinda kwasababu Atletico Madrid wameshindwa, hii ni kauli ya moja kwa moja na pia ni kauli tata ikitegemeana na wewe uko upande gani, ushindi wa leo wa Barcelona umetokana na makosa ya Atletico zaidi kuliko ubora wao ule ambao hasa unafahamika.
2. Kinyume cha hatari za MSN ni ubovu wa Pique na wenzake, kama Atletico wangekuwa makini zaidi eneo la mbele basi shughuli ya robo fainali ingeishia Nou Camp, ukuta wa Barcelona unabebwa zaidi na "ball possession" yaani timu kumiliki mpira zaidi kuliko ubora wao.
3. Luis Suarez, "Malaika na shetani" kwa wakati mmoja, hali ya Barcelona ilipokuwa dhofu mbele ya lango ushetani wa Suarez ulianza kujionyesha kwa kufanya vitendo visivyo vya kiungwana lakini dakika chache baadaye akageuka "Malaika" kutupia magoli mawili na kuipa ushindi Blaugrana.
4. Unataka show, unataka udambwiudambwi, unataka madoido, nenda kwa Neymar, ila kama unataka magoli mtafute mwingine kwenye ule utatu mahiri, bado Neymar ana kazi ya kuwa "clinical" kwenye eneo la mwisho kama leo angekuwa hivyo basi angeondoka na mpira wake.
5. "Hero and Villain" maneno mawili yenye kuonyesha mpira usivyokuwa na adabu, dakika ya 25 Torres alikuwa (hero) shujaa mbele ya Atletico na dakika ya 35 mshikaji akageuka (villain) mkosaji, mjinga, mpuuzi yani vivumishi vyote vibaya kwa kukubali kadi nyekundu ya kijinga kabisa kumjia.
6. Kikosi cha kwanza cha Barcelona ni dhahiri shahiri wanaonekana kuchoka na hasa ukizingatia kwamba juzi tu wamecheza mchezo wa el clasico na pia tabia ya kocha wa Barcelona kutokufanya "rotation" ya kikosi.
7. Namsifu kocha wa Atletico kwa "game plan" nzuri ambayo kama sio makosa ya kijinga ya Torres basi timu ingeweza kupata matokeo ya kuridhisha Nou Camp, kuikabia Barcelona kwenye eneo lao la juu haikuwa jambo rahisi lakini Atletico waliweza na kupata goli la ugenini.
8. Mpaka sasa wameshindwa mapigano lakini sio vita (losing the battle but not the war), kama wakiweza kuizuia Barcelona (MSN) wasipate goli pale Vicente Calderon basi tunaweza kuwakuta nusu fainali kinyume na hapo sioni ni kwa namna gani wataweza kuibuka na ushindi na kuwazuia MSN wasiingie nyavuni.



0 comments:
Post a Comment