Kuna namna mbalimbali ya
kusupport harakati, unaweza ukabeba bango lako mwenyewe, au siku hizi
teknolojia, unaweza ukaingia zako tu Twitter halafu unaweka hashtag,
basi unakuwa umetoa support yako ya nguvu.Hawa jamaa wa Uturuki wameona
isiwe tabu, wameingia zao na wenyewe mtaani wakiwa wamevaa zao sketi za
wanawake ili tu ku show support yao ya nguvu kwa wanawake ambao walikuwa
wakiandamana kulaani mauaji ya mwanamke mmojaOzgecan Aslan ambaye aliuawa na mwanaume aliyetaka kumbaka.
Wanawake wakaingia mtaani
kudai haki zao kwa kuwa kitendo hicho kilionyesha ukatili na unyanyasaji
wa wanawake kwa hali ya juu, wanaume wanaosupport nao wakaongeza nguvu
kwa kuvaa sketi pia na kuandamana.
Wababa na sketi zao kwenye maandamano.
Hawa huenda majukumu yaliwabana wakashindwa kuingia mtaani kuandamana, basi wakatupia PICHAZ na sketi zao mitandaoni.


0 comments:
Post a Comment