Ubora wa ligi kuu ya Hispania umekuwa unathibitishwa na uwezo
unaoneshwa na vilabu vya Real Madrid, Atletico Madrid, Villarreal na
Sevilla katika michuano ya bara la ulaya – Champions League na Europa
League wiki iliyopita.
Sare ya 0-0 ya Manchester City dhidi ya Los Blancos yanawapa nafasi zaidi vijana wa Zinedine Zidane katika mchezo wa pili wa marudiano utakaofanyika wiki hii kuelekea fainali ya Champions League mnamo May 28. Lakini mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa upande wa Atletico Madrid ambao watasafiri mpaka Allianz Arena kucheza vs Bayern Munich. Pamoja na kwamba wanaenda Ujerumani na ushindi wa 1-0 shukrani kwa goli la Saul na safu yao nzuri ya ulinzi yenye rekodi bora inaweza kuwasaidia kuvuka.
Katika
Europa League, Sevilla walifanikiwa sare ya 2-2 ugenini huko Ukraine
dhidi ya Shakhtar Donetsk na wana imani wanaweza kushinda mechi ya
marudiano nyumbani kwao katika dimba la Sanchez Pizjuanna kufuzu kwenda
fainali ya tano katika historia yao ya michuano.Villareal kwa upande
mwingine, wanaenda Anfield wakiwa mbele kwa goli moja walilofunga dakika
ya mwisho ya mchezo. Itakuwa sio rahisi kushinda Anfield, na ukiangalia
matokeo ya nyumbani ya Liverpool hasa katika michuano hii, utaona
kikosi cha Jurgen Klopp kinaweza kubadili matokeo.

Ikitokea timu zote za Hispania zikafanikiwa kuingia kwenye fainali za michuano hii mikubwa miwili ya ulaya, oitakuwa ndio mara ya kwanza kwa fainali za michuano hiyo kuhusisha timu za kutoka kwenye ligi moja. Katika historia ya Champions League, kumekuwepo na fainali nne za timu kutoka taifa moja. Hata hivyo, katika misimu hiyo hakujawahi kutokea kukuwepo fainali ya Europa league iliyohusisha timu kutoka taifa moja pia.
Namba
ya juu zaidi ya idadi ya timu katika fainali za UCL na Europa ni timu
tatu, jambo hilo lilitokea, msimu wa 1989-90, 1994-96 na 1997-98 wakati
vilabu vitatu kutoka Italia vilipokutana kwenye fainali zote mbili.
Vilabu vitatu vya Ujerumani navyo vimewahi kuingia katika fainali hizo
mbili kwa pamoja msimu wa 1979-80, wakati msimu wa 2013-14, vilabu
vitatu vya Spain vilicheza kwenye fainali hizo mbili za michuano ya
ngazi ya juu ya ulaya.
Sare ya 0-0 ya Manchester City dhidi ya Los Blancos yanawapa nafasi zaidi vijana wa Zinedine Zidane katika mchezo wa pili wa marudiano utakaofanyika wiki hii kuelekea fainali ya Champions League mnamo May 28. Lakini mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa upande wa Atletico Madrid ambao watasafiri mpaka Allianz Arena kucheza vs Bayern Munich. Pamoja na kwamba wanaenda Ujerumani na ushindi wa 1-0 shukrani kwa goli la Saul na safu yao nzuri ya ulinzi yenye rekodi bora inaweza kuwasaidia kuvuka.

Ikitokea timu zote za Hispania zikafanikiwa kuingia kwenye fainali za michuano hii mikubwa miwili ya ulaya, oitakuwa ndio mara ya kwanza kwa fainali za michuano hiyo kuhusisha timu za kutoka kwenye ligi moja. Katika historia ya Champions League, kumekuwepo na fainali nne za timu kutoka taifa moja. Hata hivyo, katika misimu hiyo hakujawahi kutokea kukuwepo fainali ya Europa league iliyohusisha timu kutoka taifa moja pia.
Namba
ya juu zaidi ya idadi ya timu katika fainali za UCL na Europa ni timu
tatu, jambo hilo lilitokea, msimu wa 1989-90, 1994-96 na 1997-98 wakati
vilabu vitatu kutoka Italia vilipokutana kwenye fainali zote mbili.
Vilabu vitatu vya Ujerumani navyo vimewahi kuingia katika fainali hizo
mbili kwa pamoja msimu wa 1979-80, wakati msimu wa 2013-14, vilabu
vitatu vya Spain vilicheza kwenye fainali hizo mbili za michuano ya
ngazi ya juu ya ulaya.

0 comments:
Post a Comment