https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Serikali yatangaza kumfungia msanii Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Wimbo wake wa Chura kutopigwa redioni na kwenye runinga.



    Katikati ni mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiwa na maafisa wengine wakizungumza na waandishi wa habari.

    Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.

    Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.

    Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar.

    Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp.

    Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Serikali yatangaza kumfungia msanii Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Wimbo wake wa Chura kutopigwa redioni na kwenye runinga. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top