Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs
iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo
aliahidi kuwasomesha watoto 100 na aliwasihi Wanawake wanapoweka mipango
ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada
ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na
Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti
Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia
Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu
cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)
akitazama jambo liliokuwa linaendelea (halionekani pichani) pamoja na
Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Binti Foundation Johari Sadiq .
Sehemu ya watoto walioshiriki kuonyesha mitindo mbali mbali ya Mavazi pamoja na Wabunifu wao.
Makamu wa Rais Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia
masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni
za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa
Mheshimiwa
Samia ametoa kauli hiyo jana kwenye hafla ya uzinduzi wa Binti club
iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha
fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na
Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa PSPF
jijini Dar es salaam
Alisema
wanaume kama wakala wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue
ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika kuzungumzia umuhimu wa kumwinua
mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala
ya ujasiriamali.
“Tuwaingize
wanaume kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu
katika mapambano hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie
nafasi hizo tulete mabadiliko,”
alisema Makamu wa Rais na kuongeza “Penye mkusanyiko wa
watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu,
wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje.”
Aliipongeza
Taasisi hiyo ya Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali
katika suala la elimu kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu
inakuwa na ugumu zaidi kuliko
wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila
potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana
na ujanajike wake.
“Tuna kazi kubwa ya kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka,” alidokeza.
Mheshimiwa
Samia alitumia fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na
serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na
kuondoa ada katika shule
za
msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi
yao, kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo
amewashukuru
Watanzania kwa kuchangia madawati.
Aliwataka wazazi kuwatunza watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote
ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema.
Mtendaji
Mkuu wa Binti Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa
shirika hilo liliamua kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha
watoto kumudu masomo yao na
hatimaye kufikia malengo yao.
“Kwa
hiyo ukiwa na fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari,
pedi, vyote tunapokea kwa ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao
yanaweza yasitimie kutokana na
changamoto hizo,”
Kampeni
hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye
mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu
na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.
Katika
hafla hiyo iliyopambwa na onesho la mavazi la watoto Makamu wa Rais
ambaye alikubali kuwa mlezi wa Binti Foundation aliahidi kusomesha
watoto 100 wakati mke wa Waziri
Mkuu, Mary Majaliwa alitoa ahadi pia ya kusomesha watoto 50.







0 comments:
Post a Comment