Bado Yanga wanaendelea kuusaka ushindi wao wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
Baada ya kupoteza mechi yao kwanza ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, leo walikuwa nyumbani wakikipiga dhidi ya TP Mazembe mchezo uliomalizika kwa Yanga kupoteza tena kwa goli 1-0.
Goli la Mazembe lilitokana na mpira wa adhabu ndogo baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Thomas Ulimwengu nje kidogo ya eneo la hatari. Mpira wa adhabu ndogo ulimfikia Merveille Bope na kuupachika kambani baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuuondosha kwenye eneo lao la hatari.
Yanga-mechi 2 bila goli
Tayari Yanga imeshacheza mechi mbili kwenye hatua ya makundi, wamefungwa zote kwa goli moja (kila mechi) huku wao wakiwa bado hawajafunga bao hata moja katika mechi walizocheza.
Chirwa, Mahadhi, mambo poa
Nyota hawa wa Yanga walikuwa wanacheza mechi yao kwa mara ya kwanza wakiwa Yanga huku Mahadhi akicheza mechi ya kwanza ya kimataifa.
Wote kwa pamoja wameonesha uwezo mkubwa kwa muda waliopata nasi ya kucheza. Mahadhi aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya huku Obrey Chirwa yeye nafasi yake ilichukuliwa na Matheo Athony.
Mazembe wamecheza kwenye uwanja wao wa nymbani
Licha ya TP Mazembe kucheza ugenini, imepata support kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao kwa muda mwingi walikuwa wakiishangilia hasa wakati mpira ukifika kwa Ulimwengu.
Yanga pia walipata nguvu kutoka kwa mashabiki wao ambao walifurika kwa wingi kuishangilia timu yao hasa kutokana na kuingia bila kulipia kiingilio baada ya uongozi wa timu yao kutangaza mchezo huo hautakuwa na kiingilo.
0 comments:
Post a Comment