Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela (pichani juu) amesema amekwisha zungumza na makundi mbalimbali ya Vijana katika ndani ya Wilaya hiyo na kukubaliana kutoshirikia maandamano ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) japo anayehitaji kuandamana ruksa ila aandamane ndani ya nyumba yake kuzunguka kitanda na sio kutoka mitaani.
Akizungumza na vijana katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa, wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Figisu ya Ndoa, Mh. Kasesela ,mkuu huyo alisema kuwa vijana wanapaswa kufanya kazi za kuwapatia kipato na sio kutumikishwa kufanya maandamano hayo ambayo kwao hayana faida yeyote.
“Tumejipanga kuwashughulikia wote watakaokaidi agizo la Serikali kuhusu maandamano ya UKUTA. Kama mtu yeyote ana hamu ya kufanya maandamano afanye ndani ya nyumba yake na kuzunguka kitanda chake na sio nje mara baada ya kumaliza kufanya maandamano ndani kwake anapotoka nje ni kwa ajili ya kwenda kufanya kazi itakayomuigizia kipato na sio kwenda vijiweni ama kwenye maandamano ya UKUTA.
Ole wake mtu akutwe akiandamana ama kupanga kuandamana “alisisitiza Mh. Kasesela.
Aidha, ameelezeza kuwa, Serikali iliyopo madarakani ni serikali yenye uchungu na maisha ya watanzania na kuwa moja katika ya mikakati yake ni kuona kila mtanzania anakuwa na maisha bora na hakuna njia ya mkato ya kuyafikia maisha bora zaidi ya kufanya kazi na sio kutumika kufanya maandamano ya kuvutana na Serikali.
Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha kuwa, tayari amekwisha pata taarifa za mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye ameendelea kuhamasisha vijana kufanya maandamano kwenye maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo na kuwa mipango yote tayari ameipata na hatua dhidi ya kiongozi huyo zinafanyika japo amesema mpango wao huo katika Wilaya ya Iringa hautafanikiwa.
” Wakati Serikali imezuia mtu ama chama chochote cha siasa kufanya mikusanyiko siku ya Septemba mosi mwaka huu, Yupo mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye anaendelea kusambaza ujumbe kwa ajili ya kuandaa maandamano ya UKUTA. Nasema hakuna aliyejuu ya sheria, Tutashughulika na uvunjaji huu wa sheria unaofanywa na kiongozi huyo” Alisisitiza Mh. Kasesela.
Aidha aliwataka vijana kutokubali kuingizwa katika matatizo na kiongozi mmoja mwenye lengo baya dhidi yao na badala yake kupuuza wito wake na kuendelea na shughuli zao za kila siku .
Kasesela amesema amepata kufanya vikao na makundi mbali mbali kwa kuwashirikisha baadhi ya madiwani wa Kata wakiwemo wa Chadema na wameapa kutoshiriki maandamano hayo.
0 comments:
Post a Comment