Siku
kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kutengenezwa kwa basi la umeme
lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine huko China. Kutokana na
China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo
linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari barabarani, imeelezwa kuwa basi hilo tayari limevutia serikali za Brazil, Ufaransa , India na Indonesia.
Hii ndio
mara ya kwanza kwa wabunifu hao kuonesha basi hilo hadharani baada ya
video yake kuvuja katika mitandao mwezi May, wiki hii basi hilo
limefanyiwa majaribio kwenye eneo la kaskazini mwa China jimbo la Hebei
katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300, basi
hilo lina uwezo wa kuhudumu kwa kasi ya kilometa 60 kwa saa na litakuwa
na uwezo wa kubeba watu 1200 kwa wakati mmoja.


0 comments:
Post a Comment