Na Athumani Adam
Tetesi zimekuwa kweli mapema wiki hii pale Arsene wenger
alipokamilisha usajili wa beki Shkodran Mustafi. Usajili wa beki huyo
Mjerumani mwenye miaka 24 kutoka klabu ya Valencia ya kule nchini
Hispania utasaidia kuziba nafasi zilizopo kwenye safu ya ulinzi ya
Arsenal ukizingatia Per Mertesacker bado anasumbuliwa na majeraha
Ikiwa bado mashabiki wa Arsenal wana furaha ya ujio wa Mustafi, makala hii inakupa historia fupi kabla ya kuja Arsenal
- HISTORIA
Shkodran Mustafi alizaliwa tarehe 17 April 1992 kule Bad Hersfeld
nchini Ujerumani. Wazazi wake ni raia wa Albania wenye asili ya
Marcedonia. Mwaka 2006 alijiunga na timu ya vijana ya Hamburger SV
- AKATAA OFA YA MAN CITY NA NEWCASTLE
Mwaka 2009 klabu za Man City pamoja na Newcastle United zilitaka
kumsajili Mustafi lakini akataa na kuelekea zake kule Merseyside kwenye
klabu ya Everton
- ACHEZA GAME MMOJA TU EVERTON
Tangu ajiunge na Everton hadi anaondoka mwaka mwaka 2012, Mustafi
alicheza mechi moja tu. Mechi ambayo Mustafi alicheza ilikuwa dhidi ya
Bate Borisov michuano ya Europa League. Ilikuwa kwenye uwanja wa
Goodson Park December 16, 2009 mchezo ambao Everton ililala 1-0
Baada ya kuona hapati nafasi ya kutosha kucheza, mustafi alimwomba
kocha David Moyes kuhama Everton na kulelekea kwenye klabu ya Sampdoria.
- AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA SAMPDORIA (MECHI 53, GOLI 1)
Mustafi alifunga goli lake la kwanza kama mchezaji “professional”
kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Atlanta October 2013. Sampdoria ilikuwa
imepanda daraja kutoka Serie B tangu iliposhuka mwaka 2011. Mbali na
Mustafi pia Samporia walikuwa na wachezaji vijana Simon Zaza na Mauro
Icardi
- DAU LA USAJILI LAWA SIRI VALENCIA (MECHI 78, GOLI 6)
Mustafi alijiunga na Valencia mwaka 2014 akitokea Sampodria bila dau
la usajili kuwekwa wazi. Zipo tetesi kwamba japo haikuwekwa wazi, lakini
Mustafi alitua kwa Euro milioni 8. Ndani ya Valencia Mustafi alicheza
mechi 78 na kufunga goli 6.
- ALIKUWEPO WORLD 2014, EURO 2016
Mustafi alikuwepo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la
dunia kule nchini Brazil mwaka 2014. Alipata kuitwa kwenye kikosi na
kocha Joackim Low baada ya kuumia kiungo Marco Reus. Mustafi aliingia
kutokea sub kwenye mechi dhidi ya Portugal na Ghana. Bahati mbaya
aliuumia wakati mashindano yanaendelea
Mbali na kombe la dunia pia mustafi alikuwepo kwenye mashindano ya euro 2016 kule nchini Ufaransana.
0 comments:
Post a Comment