https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Tigo yaanzisha mkakati wa huduma kwa jamii nchi nzima katika msimu wa Fiesta 2016

    Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo,wakati wa hafla iliyofanyika jana.



    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(wa tatu kulia) akimpa mkono Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya,kwenye hafla ya kukabidhi madawati 60 kwa Shule ya Msingi Bwiru jana.



    •Shule 9 za msingi Mwanza zapokea madawati 385
    Mwanza, Agosti 19, 2016:   Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo  imeanzisha rasmi  mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii  kwa kuchangia madawati 385  yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza  ambayo  yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za  Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza
    Kukabidhiwa kwa madawati hayo mkoani Mwanza ni matokeo ya juhudi zinazoendelea za Tigo za kuwekezaq katika  elimu na hususani katika kupunguza uhaba wa madawati  katika shule za msingi za umma nchi ambapo  mikoa 18 itanufaika katika msimu wa Fiesta 2016. Ikumbukwe kwamba kwa mwaka huu  kampuni imeshachangia madawati 5,700 kote nchini na hivyo kuwa imewakalisha wanafunzi 17,000 ambao awali walikuwa wakikaa sakafuni.
    Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’
    Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo  zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bwiru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya, alisema  uhaba wa madawati katika shule za msingi unajulikana kama moja ya sababu zinazoathiri kujifunza  pamoja na ufanisi wa wanafunzi  katika  shule zetu nyingi za msingi.
    “Tumejikita katika kuhakikisha kuwa mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi yanaboreshwa  na tunayofuraha  kwamba Tigo inabadilisha kizazi cha baadaye  am,bacho ni wanafunzi katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai chini tena. Tunaamini  kwamba msaada huu utaenda mbali katika kuwasadia wanafunzi kuzifikia ndooto zao za kuwa viongozi wa baadaye kutokana na kuondoka kwa bughudha  na hivyo kujikita katika masomo,” alisema Maswanya.
    Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye alisema kuwa madawati 385 yataboresha kwa kiwango kikubwa  mazingira ya kujifunza  kwa watoto katika mkoa huo  na kuwataka  watu wengine wenye mapenzi mema  kujitokeza  na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mkoa huo.
    Mongela alizitaja shule zitakazopokea madawati hayo na idadi katika mabano kuwa ni  Nakoza (29), Uhuru (40), Busangu (41), Bukongo (30), Nansio (30), Namagubho (30), Mkuyuni (65) Chambanda (60) na Bwiru (60) .
    “Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza kiasi cha uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Mwanza. Tunaamini  madawati haya 385  yatatufikisha mbali  katika  kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio  katika elimu yao,” alisema Mongela.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Tigo yaanzisha mkakati wa huduma kwa jamii nchi nzima katika msimu wa Fiesta 2016 Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top