Mkutano wa mkuu wa Umoja wa Mataifa, United Nations General Assembly (UNGA) umeanza wiki hii nchi Marekani katika jiji la New York,
na kushuhudiwa viongozi wa mataifa mbalimbali wakihutubia mkutano huo
utakaojadili masuala makubwa yanayoikabili dunia kwasasa ikiwemo suala
la wakimbizi, utawala wa haki na demokrasia, uchumi na mengineyo.
Kupitia hotuba aliyoitoa Rais wa Marekani Barack Obama
ameyataka mataifa tajiri kufanya kila linalowezekana kuwasaidia watu
wanaokimbia vita huku akikiri kuwa dunia inakabiliwa na changamoto
nyingi na kuzitaka nchi tajiri
kuchukulia tatizo hilo kama ni lao huku akisema kuwa ongezeko la
wakimbizi ni ishara ya vita na mateso na kwamba hali hiyo itaweza
kushughulikiwa tu endapo migogoro kama ule wa Syria itamalizwa.
Huu unakua mkutano wa mwisho kwa viongozi wakubwa wawili ambao ni Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambao wanahudhuria vikao hivyo kwa mara ya mwisho wakiwa madarakani.
0 comments:
Post a Comment