Grande Hotel katika mji wa Beira pwani ya Msumbiji inahifadhi maskwota
3,500. Mpiga picha Fellipe Abreu alitembelea mjengo huo ambao kwa wakati
mmoja uliitwa "Fahari ya Afrika":
Watu kwenye ngazi ya Grande Hotel katika mji wa Beira pwani ya Msumbiji
Ilipofunguliwa 1955, ilikuwa nimojawapo ya hoteli za kifahari Afrika. Ni jengo lenye orofa 3…
... Dimbiwi la kuogolea - sasa linatumika kufuwa nguo - ngazi ndefu,maduka, migahawa, ofisi ya posta, sinema, na vyumba 122.
Ilitarajiwa pia kuwa na sehemu ya
kucheza kamari, lakini wamiliki walishindwa kupata kibali kutoka kwa
maafisa wa kikoloni wa Ureno.
Hapa ndipo matatizo yalipoanza licha
ya kuwa Beiran ni mji maarufu wa pwani ya bahari hindi, hoteli haikuweza
kuvutia wageni wengi.
Ilifungwa 1963 na ilitumika kwa hafla na sherehe kubwa pekee.
Wakati wa vita vya kiraia mwishoni mwa miaka ya 70, ilikuwa kambi ya jeshi na gereza kwa wafungwa wa kisiasa.
Baada ya kufungwa kwa hoteli hiyo katika mwongo uliofuata iliporwa na watu wakaingia kuishi hususan waliokuwa wanatoroka vita.
Kwa mara ya kwanza, hoteli ilijaa
watu. Kwa sasa imezidi kima chake cha kawaida wakati familia wanaishi
katika kila sehemu ya hoteli hiyo yenye kiza, na joto jingi, ikiwemo
wanaoishi kwenye ngazi.
Kumetengenezwa sehemu ya burudani ya
kutizama filamu katika sehemu ya pekee ilo na umeme katika hoteli hiyo.
kwa kawaida kuna watoo na watu wazima wanaokaa kutizama TV
Baadhi ya familia sasa wanaishi katika
hoteli hiyo kwa vizazi vitatu. miaka 24 tangu kumalizika vita vya kirai
, zaidi ya idadi nusu ya raia Msumbiji wanaendelea kuishi katika
umaskini.
Kwasababu hoteli hiyo haitizamwi, jengo lina matatizo huku miti ikimea juu.
Usafi pia ni tatizo , taka za miaka kadhaa zimekusanyika na mgahawa mmoja unatumika kama choo siku hizi.
Mkaazi huyu anaikarabati hoteli hii, ana anatengeneza matofali ya kukarabati eneo lililo chomeka na moto.
Watu wanaoishi Grande Hotel hawalipi
kodi , lakini kumewekwa sheria na hakuruhusiwi wakaazi wapya kwasababu
wanasema hoteli imejaa.
Viongozi wa jamii katika eneo hilo,
kama Carlos Nori (kwenye picha), wanachaguliwa na wakaazi na kuna baraza
linalokutana kila mwezi kujadili matatizo yoyote
Na pia wanapanga michezo. "karibu kila siku, wanaume hukutana nje na kucheza soka," anasema bwana Nori.
0 comments:
Post a Comment