ENEO
la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa
kitovu cha biashara hapa nchini eneo hilo litasaidia kwa kila
mfanyabiashara kuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na
kuitumia ipasavyo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard
Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo, Amesema kuwa hiyo ni moja ya Mkakati wa harakati za kuhakikisha
kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati.
Katika
kuhakikisha kwamba kodi ya ongzeko la thamani VAT inakusanyawa kwa
Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya
Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla ya
tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka
huu wa fedha.
Kayombo
amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeanza kuonyesha
mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi
Agosti 2016 imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la
Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti Mwaka
2015 TRA ilikusanya Billion 923.
Pia
Kayombo ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki
taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika
vituo TRA vilivyo karibu kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo.
Amesema kuwa vituo vya kuhakiki taarifa zao ni pamoja na vitua vya
• Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
• Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara
• Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
• Wilaya ya Kigamboni - Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja
na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini
wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili
kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na
uhamasishaji.
Kayombo
pia amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la
Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla Septemba 30 mwaka huu kwani
kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe Oktoba 1 na
hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka
agizo hilo.
Na
walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo
wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli
za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Baadhi
ya waandishi wa Habri wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
0 comments:
Post a Comment