FC Barcelona ambao walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani walipata pigo katika mchezo huo ambapo mchezaji wao tegemeo Lionel Messi aliumia mguu wake wa kulia dakika ya 51 na kutolewa nje na nafasi yake kuchuliwa na Arda Turan.
Leo Septemba 22 2016 taarifa zimetoka Lionel Messi atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu na atakosa michezo sita dhidi ya Sporting Gijon, Gladbach, Celta Vigo, Deportivo la Coruna na anatazamiwa kuwa fiti katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Man City October 19 2016.
0 comments:
Post a Comment