VIJANA saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo Jumamosi.
Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
Katika majaribio hayo walijitokeza vijana 433 wenye umri tofauti kuanzia chini ya umri wa miaka 10, 12, 14 na 17, ambapo waliweza kuchaguliwa saba pekee na wengine 33 kuorodheshwa.
Mpaka sasa mpango huo umeshahusisha mikoa maeneo matano tofauti nchini katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma na Visiwani Zanzibar, ambako kote kumefanya idadi ya vijana waliofanyiwa usaili kufikia 2,593, kati ya hao 50 pekee ndio waliochaguliwa kushiriki fainali ya mwisho itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi ujao.
Mbali na hao 50, wengine 96 wameorodheshwa na kuhifadhiwa kama akiba ya baadaye.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, alisema kuwa amefurashishwa na vijana waliojitokeza kwenye majaribio hayo huku akidai kuwa viwango vilikuwa ni vya hali ya juu.
“Wamejitokeza vijana wadogo sana wanaotoka maeneo ya Chamazi na Mbagala, nimefurahishwa sana kuwaona viwango vilikuwa juu na kiukweli ilikuwa nji nzuri ya kumaliza majaribio Dar es Salaam,” alisema.
Alisema kuwa mara baada ya kumaliza vema zoezi hilo Dar es Salaam, hivi sasa mipango iliyopo ni kuthibitisha tarehe za majaribio mengine ya wazi kwenye maeneo yaliyobakia Tanzania.
“Kwa sasa tunachoangalia ni kwenda kwenye maeneo mengine manne kwenye mikoa ya Mbeya, Kigoma, Mwanza na tutahudhuria michuanio ya vijana Arusha Desemba mwaka huu, baada ya hapo katikati ya mwezi Desemba tutafanya fainali ya mwisho hapa Chamazi, ambayo itatoa majibu ya timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 17,” alisema.
Kwa taarifa nyingine za kina kuhusu program hii, tunakuomba uendelee kufuatilia vyanzo vyetu mbalimbali vya habari (www.azamfc.co.tz , mitandao yetu wa Facebook na Twitter ‘Azam FC’)
0 comments:
Post a Comment