Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati),
akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya
usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar
es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na
magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
Takataka zikipelekwa eneo maalumu.
Takataka zikipelekwa kutupwa.
Waumini wa kanisa hilo wakipiga picha mbalimbali za tukio hilo.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia),
akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati
alipowaongoza waumini wa kanisa hilo kutoa msaada wa magodoro na
vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam
leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga
Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa
hilo.
Kiongozi wa kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa (kulia), akipanda mti.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu (kulia), akipanda mti.
Ofisa Afya wa Hospitali hiyo, Amina Pole (kushoto),
akipanda mti.
Waumini wa kanisa hilo na viongozi wao wakiwa kwenye
tukio hilo.
Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada huo. |
Na Dotto Mwaibale
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa amesema
migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha hali ya
amani nchini.
Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kutoa misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
"Migogoro
ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa inaweza kuhatarisha amani ya
nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na kuweka mambo sawa"
alisema Mokiwa.
Alisema
migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha kutoweka kwa amani
hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo kwa karibu na
kulitafutia ufumbuzi.
Alisema
nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana na matukio ya
kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya viroba
vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.
Alisema
matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi kukimbia nchi yao kwa
hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya mungu.
Akizungumzia msaada uliotolewa na kanisa hilo katika hospitali hiyo ambao ni vitanda 15,magodoro 20, mashuka 40 na viatu vya tahadhri jozi 30 vyenye thamani ya Sh12 milioni alisema kanisa hilo kwa muda mrefu limekuwa likifanya maombi ya kuwaombea viongozi wa nchi na kutoa misaada ya kijamii hususan katika sekta ya afya, elimu na maeneo mengine.
Mokiwa
alisema wananchi wanapokuwa katika afya bora ndipo wanapoweza kufanya
shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo kuinua uchumi wao na taifa kwa
ujumla.
Mkuu
wa kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa alitoa
mwito kwa wadau wa maendeleo kote nchini kuwa na moyo wa kusaidia watu
wenye uhitaji kama wanavyotoa michango ya harusi na sherehe nyingine.
Alisema
ni jukumu la kima mmoja wetu wa kusaidia jamii na si kuiachia serikali
pekee na ndio maana kanisa hilo limekuwa likifanya hivyo kama neno la
mungu linavyoelekeza kuwa tupendane kwani unapokwenda kumfariji mgonjwa
inasaidia kumpa hali ya unafuu.
Akizungumza kwa niaba ya serikali na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu alilishukuru kanisa hilo kwa msaada huo na kusema inazidisha ari ya kazi kwa wafanyakazi na kuwafariji wagonjwa ikiwa na kuwafanya wapate nafuu na kupona haraka
0 comments:
Post a Comment