Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandamizi Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza
matambezi ya hiari sehemu ya maadhimisho ya siku ya Maadili nchini
yatakayofikia kileleni tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam na Matembeze hayo yamefanyika Leo jijini Dar
es salaam kuanzia kwenye viwanja vya Karimjee na kufikia ukomo viwanja
vya Mnazi Mmoja.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandamizi John Kijazi( mwenye koti la bluu) akishiriki
katika mazoezi ya viungo baada ya kumaliza matembezi ya hiari ambayo
yamefanyika Leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandamizi Balozi John Kijazi akiwahutubia washiriki wa
matembezi ya hiari ( hawapo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi
hayo Jijini Dar es salaam.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza
mbele ya mgeni rasmi Balozi John Kijazi (hayupo Pichani) mara baada ya
kumalizika kwa matembezi ya hiari katika viwanja vya Mnazi Mmoja na
kushoto ni Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) ambaye ni
mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maadhimisho ya Haki za Binadamu,Bw.Valentino
Mlowola akifafanua jambo mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya
Hiari yaliyomalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja katikati ni Katibu Mkuu
Balozi Kijazi.
Kaimu
Kamishna wa Maadili Bw.Waziri Kipacha akitoa neno la shukrani kwa mgeni
rasmi Balozi John Kijazi kwenye Matembezi ya Hiari baada ya kumaliza.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ( Mwenye koti la bluu) akiwa kwenye
picha ya pamoja nabaadhi ya viongozi na watumishi kutoka Taasisi
zinazosimamia Maadili,Uwajibikaji,Utawala Bora,Haki za Binadamu na
Mapambano dhidi ya Rushwa baada ya kumalizika kwa matembezi ya Hiari
ambayo ni sehemu za Maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yanayotarajia
kufikia kileleni Desemba 10,2016 viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya
pamoja na watoto ambao waliungana na watumishi katika Matembezi hayo
yaliyofanyika Leo.
Picha Zote na Ally Mataula-Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
...........................................................
Na Alex Mathias na Joseph Ishengoma
Serikali
ya awamu ya tano imesema kuwa imedhamiria kwa dhati kupambana na
rushwa za kila aina ili kujenga jamii yenye maadili na inayochukia
vitendo vya rushwa kwa kufuata kauli ya Rais wa Tanzania anayekemia
Rushwa nchini.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Mwandisi Balozi John Kijazi amesema hayo leo jijini
Dar es Salaam wakati akihitimisha matembezi ya watumishi wa taasisi
zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na
mapambano dhidi ya rushwa yaliyoanza mapema Asubuhi katika viwanja vya
Karimjee na kufikia mwisho viwanja vya Mnazi Mmoja ambayo yaliweza
kuzishirikisha Taasisi mbalimbali zinahusiana na masuala ya utawala bora
kwa mara ya kwanza kukutana.
Taasisi
hizo ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, taasisi ya kuzuia
na kupambana na rushwa, mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma, na ofisi
ya Taifa ya ukaguzi wa hesabu ambazo zilikuwa hazijawahi kukutana
kufanya matembezi kama hayo nyingine ni Ofsi ya Rais,Utumishi na Utawala
Bora,Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Haki za Binadamu.
“Ipo
mifano ya sehemu ambazo rushwa imekithiri kutokana na vitendoi vya
rushwa na ufisadi. Kiongozi mkubwa anashindwa kumsimamia mtu aliyechini
yake kama sheria ya maadili inavyomtaka kwasababu yeye mwenyewe mikono
yake si misafi,” amesema na kuongeza kuwa , “matokeo yake hata mtu awe
na mali nyingi, bado ataendelea kula rushwa bila kikomo”.
“Serikli
ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na rushwa ya aina zote kwa lengo
la kujenga jamii yenye maadili inayochukia vitendo vya rushwa na
ufisadi ili kuweza kuondoa rundo la rushwa ambalo lilikuwa limeanza
kuikumba nchini kwa baadhi ya watumishi kujihusisha na masuala ya
Rushwa.”amesema Balozi Kijazi
Kwa
mujibu wa Balozi Kijazi, jitihada za serikali ni kuondokana na hulka
ya ubinafsi na uroho na kujenga utamaduni na tabia ya kijitolea kwani
hata awamu hii ya Rais Magufuli inapambana na janga hilo ndio maana kila
Wizara imekuwa makini kwa watumishi wake na kuwaonya kuacha mara moja
kujihusisha na Rushwa nchini
Aidha
Katibu Mkuu Kiongozi ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya
habari kuonyesha uzalendo kwa kuielimisha jamii kuhusu maswala ya
maadili nchini kwa kuandika ukweli wa mambo ili kuweza kufikisha ujumbe
katika jamii zetu na kuunga mkono kauli hii ya kupiga Rushwa.
“Natoa
wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo
kwa taifa letu kwa kuielimisha jamii kuhusu kujenga, na kukuza maadili,
haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa
ili kuandika makala ambazo zinaonesha ukweli wa kuwaelimisha wananchi
kwa nguvu zote na kuweza kuwa na jamii bora ambayo haina uroho wa
Madaraka,” amesema.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna
Valentino Mlowola ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutuma ujumbe
kwa wananchi kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu,
uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.
Kamishna
Mlowola amesema, kuanzia Jumatatu ijayo, taasisi zinazohusika na
masuala ya utawala bora zitakuwa na wiki ya utoaji huduma katika viwanja
vya Mnazi Mmoja ili kupokea kero na malalamiko ya wananchi na kisha
kuyashughulikia pamoja na kuyatatua kwa umakini kwa kufuata haki za kila
binadamu ili aweze kusaidiwa ikiwa ana kero ambayo inamuumiza katika
jamiii.
“Hii
ni moja ya kampeini ya taasisi husika kuikataa rushwa, kujenga maadili
na misingi ya uadilifu na kuhamasisha jamii kujua haki zao,” amesema.
Matembezi
ya Leo ni ya mwendelezo wa Kampeni ya maadhimisho ya siku ya maadili
na haki za binadamu ambayo yalifunguliwa Novemba 10 mwaka huu na
yanatarajia kufikia kilele chake Desemba 10,2016 na pia amewataka
watumishi waendelee kufanya mazoezi ili kujiweka fiti na sio kukomea
siku ya Leo tu.
0 comments:
Post a Comment