Barua iliyowekwa sahihi na
mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa Afrika
Kusini Nelson Mandela, akitoa rambu ramba zake kufuatia kuawa kwa mtu
aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200.
Muuzaji
wa barua hiyo Andrew Aldridge alisema, "ni vyema kuwa Mohammad Ali
alikuwa mwanamichezo bora zaidi hukui naye Nelson Mandela akiwa mtu
mashuhuri zaidi katika karne iliyopita.Barua hiyo ilipiwa chapa cha msaidizi wa meneja wa hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo.
Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekania ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.
Muhammad Ali alikuwa nchini Afrika Kisini kwa kipindi kifupi mwezi Aprili mwaka 1993 baada ya kuwasili muda mfupi baada ya kuuliwa kwa Chris Hani tarehe 10 mwezi Aprili.
Hani alikuwq kamanda wa kundi la Umkhonto We Sizwe, kundi lililojihami la ANC.
Alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi na aliuaw mkereketwa mmoja nje ya nyumba yake eneo la Boksburg.
0 comments:
Post a Comment