DARASA AISIMAMISHA ILALA KWA SHOO KALI
MWANAMUZIKI
wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet
‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki
wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa
Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Darassa
na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa
Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano
la Nichane Nikuchane.
Akiwa
kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala
pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili
ya siku hiyo.
Akizungumza
na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya
Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar
Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa
nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”
Naye
Meneja wa Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah
Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama
tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye
Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye
Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku
hiyo.”
Katika
hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma
Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya
kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7
mchana mpaka majogoo.”
Mbali na
wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani
ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature,
Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment