https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    KUIDHINISHWA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA GHANA

    Waangalizi wa ndani katika uchaguzi uliopita wa Bunge na Rais katika nchi ya Ghana ya magharibi mwa Afrika wameunga mkono na kuidhinisha matokeo ya uchaguzi huo.
    Uchaguzi wa Rais na Bunge nchini Ghana ulifanyika Jumatano ya tarehe 7 mwezi huu ambapo kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo, Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic NPP, aliibuka mshindi katika uchaguzi huo huku chama chake kikilidhibiti Bunge baada ya kupata viti vingi. John Dramani Mahama ambaye alishika hatamu za kuiongoza nchi hiyo Julai mwaka 2012 baada ya kuaga dunia Rais John Atta Mills na kisha kushinda katika uchaguzi mdogo wa 2013, alibwagwa na mgombea wa upinzani Nana Akufo-Addo ambaye alikuwa anawania kiti cha urais kwa mara ya tatu. Katika chaguzi mbili zilizopita za mwaka 2008 na 2012, Akufo Addo alikuwa akishindwa na mpinzani wake kwa uchache wa kura.
    Rais wa sasa wa Ghana (kushot) na Rais mteule Nana Akufo Addo
    Rais mteule wa Ghana ambaye aliibuka na ushindi wa asilimia 53.8 katika uchaguzi uliopita mara hii alifanikiwa kumbwaga Mahama na hivyo kuhitimisha hatamu za uongozi za chama tawala nchini Ghana. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, safari za kampeni za nchi nzima alizofanya Nana Akufo Addo wakati wa kampeni zake za uchaguzi kwa ajili ya kutafuta kura zilikuwa na taathira katika kumpatia ushindi. Ahadi za mwanasiasa huyo za kuandaa fursa za kazi kwa ajili ya vijana, kuwashajiisha wawekezaji wa kigeni kwenda nchini humo na kubadilisha hali ya uchumi ya nchi hiyo  nazo zinatajwa na wajuzi wa mambo kwamba, zilimpiga jeki mno na kumuongeza idadi ya kura zake.
    Wajuzi wa mambo wanaamini kwamba, ukuaji wa mwendo wa kinyonga wa uchumi wa Ghana, ughali wa maisha, mzigo wa madeni ya serikali na kupungua thamani ya Cedi ambayo ndio sarafu rasmi ya nchi hiyo ni sababu zilizopelekea wapiga kura kumchagua kiongozi wa upinzani. Katika hali ambayo baada ya Afrika Kusini  Ghana inahesabiwa kuwa ni nchi ya pili kwa usafirishaji dhahabu nje ya nchi na ni ya pili pia kwa usafirishaji kakao barani Afrika baada ya Ivory Coast, mwaka jana serikali ya Accra ilichukua mkopo wa thamani ya dola milioni 918 kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF.
    Zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa Disemba 7, 2016
    Wataalamu wa mambo wanaamini kwamba, kupungua kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Ghana ambao katika miongo miwili ya hivi karibuni umeporomoka mno na kufikia kiwango cha chini zaidi ni jambo ambalo limechangia kupungua mapenzi na uungaji mkono wa wananchi wa nchi hiyo kwa chama tawala cha The National Democratic Party (NDP). Katika uchaguzi wa mara hii, Rais Mahama aliambulia asilimia 44.14 ya kura za urais.
    Rais mteule wa Ghana Nana Akuffo Addo ambaye ni mwanasheria anatoka katika mji wa Kyebi wa mashariki mwa nchi na katika familia ambayo ni mashuhuri kwa kutoa shakhsia wenye vipawa vya kisiasa. Akihutubia kwa mnasaba wa kuibuka na ushindi, Rais mteule wa Ghana aliwakosoa vikali viongozi wa magharibi mwa Afrika wenye tamaa na uchu wa kung'ang'ania madaraka.
    Rais mteule wa Ghana Nana Akufo Addo
    Nana Akufo Addo alitoa matamshi hayo ya ukosoaji katika hali ambayo, Rais wa Gambia Yahya Jammeh amewashangaza wengi baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa nchi hiyo ambayo awali aliyakubali. Kuidhinishwa matokeo ya uchaguzi wa Ghana ni ishara ya kuimarika demokrasia katika nchi hiyo. Baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi, Rais Mahama alitangaza kukubali kushindwa na kumpongeza mshindani wake kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Ghana. Aidha alisema kuwa, kukabidhiwa madaraka kwa njia ya amani nchini Ghana unaweza kuwa mfano wa kuigwa wa kidemokrasia na utawala kwa wananchi wa bara la Afrika ambapo katika nchi nyingi za bara hilo kuna mifumo ya kidikteta na tawala zilizoingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ambazo zimekuwa zikiwadhibiti kikamilifu raia wake na kuzima sauti za kupigania utawala wa demokrasia.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUIDHINISHWA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA GHANA Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top