Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti
Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji
Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa
ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ambapo aliwaambia wananchi
walishiriki kwenye tukio hilo kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya
kuonekana yupo imara ni mazoezi hivyo aliwataka wananchi wajenge tabia
ya kushiriki na kufanya mazoezi kwani kutawaepusha na maradhi mengi .
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim
akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa
ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiongoza matembezi ikiwa sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi
akiongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kabla ya
kufungua Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza
kwenye viwanja vya Leaders Club viongozi wengine walioshiriki matembezi
hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalah, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Paul Makonda .
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua
wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye
viwanja vya Leaders Club.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda
wa miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka
maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli
zao binafsi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi
na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya
kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa
kurudisha maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya
wananchi kufanya mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza.
Katika
kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na
wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara
Moja.
“Nitamke
kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa
sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha
na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa
kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”
Makamu wa
Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia
kurudisha mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.
Amesema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
“Natoa
rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja
katika Muda ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.
Katika
hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha
haraka mchakato wa kuunda kamati ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya
kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka wizara mbalimbali nchini.
Amesisitiza kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.
Kwa
upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka
sana duniani kote hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara
ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo mpaka sasa yanachangia asilimia 27
ya vifo Duniani.
Amesema
utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini
umeonyesha viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya
wananchi ni wanene kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini
na asilimia 25.9 wanashinikizo kubwa la damu.
Utafiti
huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na
asilimia 97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara
tano kwa siku.
Waziri wa
afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa
hayo kwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda
wa nusu saa, kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya
pombe kupita kiasi na kujiepusha na matumizi ya tumbaku.
Kwa
upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika
nasaha zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda
afya zao.
Amesema
kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya
neva na figo.
0 comments:
Post a Comment