Bado dunia ya soka inakumbuka na itakumbuka na kuomboleza siku zote kuhusiana na msiba wa wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil, waliyofariki kwa ajali ya ndege Colombia wakati wakielekea kucheza fainali yao ya kwanza ya klabu Bingwa America Kusini (Sudamericana) dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.
Jioni ya December 2 jina la kiungo wa timu ya Chapecoense ambaye hakusafiri na timu kuelekea Colombia Moises Santos kutokana na kuwa majeruhi amekataa kuwa wachezaji wenzake hawakupata ajali bali waliuwawa, huku mtuhumiwa namba moja akimtaja kuwa ni rubani Miguel Quiroga.
Rubani Miguel Quiroga inaripotiwa kuwa alisikia ishara na ndege ilitoa tahadhari kuwa haikuwa na mafuta ya kutosha na kuna tatizo la umeme lakini hakuwa makini na hilo, kitu ambacho kimemsikitisha Moises na kumtuhumu rubani Quiroga ambaye nae amefariki kwenye ajali hiyo amegharimu maisha ya watu wengi.
“Rafiki zangu waliuwawa ile haikuwa ajali huwezi kumuamini sana binadamu, yule jamaa aliyewabeba wachezaji wa Chapecoense uzembe wake umeharibu maisha ya familia nyingi, ameharibu mji mzima wa Chapeco itachukua muda mrefu sana watu kurudi katika hali zao za kawaida katika mji wa Chapeco”
STORI KUTOKA: Dailymail
0 comments:
Post a Comment