Miili ya watu 71 waliokufa katika
ajali ya ndege nchini Colombia, na kuleta majonzi kwa soka la taifa
la Brazil na dunia kwa ujumla inarejeshwa nyumbani kwa ajili ya
maziko.
Zaidi ya watu 100,000 wanatarajiwa
kujitokeza kwa ajili misa maalum itakayofanyika kwenye uwanja wa
Chapeco baadaye hii leo.
Watu sita tu walinusurika kifo siku
ya jumatatu, katika ajali hiyo nje ya mji wa Medellin, wakati
wachezaji wa timu ya Chapecoense walipokuwa wanaenda kucheza mchezo
wa fainali.
Rais wa Brazil Michel Temer
anatarajiwa kuwapo uwanja wa ndege kuipokea miili ya wachezaji wa
timu ya Chapecoense itakapowasili kwa ndege.
0 comments:
Post a Comment