Alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa
lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi
hiyo.
Nape
amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo
viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa
kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao
makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
"Nawaomba
msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata wapinzani pale
ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani sana. Nategemea
ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea kwa ndugu yangu
Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema Nape
Nape
pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake
kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.
"Nakiri
mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia
Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama, nilipata wosia
wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza salama"
0 comments:
Post a Comment