Akizungumza
mbele ya Wanahabari mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa
Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network
(TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika
kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha
wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema
kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa
Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye,
"Mgeni
rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni Waziri Nape Nnauye,lengo
kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo juu
ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa
kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na
mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.
Alisema
kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira
nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa
tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu
kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga
msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii,
Mkutano
huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa
mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni
mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
0 comments:
Post a Comment