Dar es Salaam – Desemba 8, 2016 –Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya MIC Tanzania Limited (Tigo) leo imetangaza rasmi kuwasilisha muhtasari na maombi ya awali katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kuhusiana na mapendekezo ya awali ya kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Uuzwaji wa hisa hizo unatarajiwa kuanza mara baada ya CMSA na DSE kumaliza mchakato wa mapitio kulingana na masharti yanayohusu soko la hisa.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez, alisema: “Tunayo furaha kutangazia umma kuhusu uwasilishaji wa muhtasari wetu ili mchakato uanze rasmi na kwamba tutawapatia wateja wetu, wafanyakazi wetu na Watanzania kwa ujumla fursa ya kuwa wamiliki wa hisa ndani ya kampuni yetu.”
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya MIC Tanzania Limited, Balozi (Mstaafu) Ami Mpungwe aliongeza kuwa: “uwasilishaji huu ni hatua muhimu katika historia ya kampuni na kwamba utawapatia Watanzania wote fursa sawa ya kushiriki katika mtaji wa kampuni yetu katika siku za usoni. Tutafanya kazi pamoja na mamlaka za usimamizi kuhakikisha mchakato huu unafanyika ipasavyo.”
0 comments:
Post a Comment