Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa pembe za faru John na Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa
Wanyamapori (Acting Assistant Director of Antipoaching, Wildlife
Division), Bw. Robert Mande, katika kikao klichofanyika kwenye Makazi
yake jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili
na Utalii, Profesa Jumanninayoelezea e maghembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Aonyeshwa pia pembe mbili za faru huyo
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa utaratibu uliotumika kumhamisha
faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino
Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana
(Ijumaa, Desemba 9, 2016) na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake,
Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi
yake.
“Nilipokea
taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza
sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa
yenu,” amesema.
Akisoma
taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia
Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na
asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.
“Kati
ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na
asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha
kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya
Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.
Baada
ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya
faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu.
Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru.
Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.
Akikabidhi
pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande
alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6
na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.
Watendaji
wa wizara waliohudhuria kikao hicho ni Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Iddi
Mfunda; Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bw.
Freddy Manongi; Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Bw. Simon Mduma; Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Bw. Alexander Songorwa na Mkuu wa Pori
la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Bw. Nollasco Ngowe.
Desemba
6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza
uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote
zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye
hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.
Alitoa
agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani
Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo
pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya
kikazi mkoani humo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, DESEMBA 9, 2016.
0 comments:
Post a Comment