Wananchi
wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa
wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na
Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali
halisi ya mgogoro uliopo .
Magari
yaliyokuwa yamebeba wajumbe wa kamati hiyo yakiwa yameegeshwa baada ya
wananchi kuzuia msafara huo wakishikiza kamati kusikiliza kero
walizokuwa nazo.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wa kuzungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
Mbunge wa
Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii
ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati
hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya
Kaskazini.
Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha
Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia
kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza
kusikilizwa kero zao.
Katika Pori tengefu la Loliondo
lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro uliodumu
kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo
kikitafutiwa ufumbuzi.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo
la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa
njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa
wamezuia barabara
Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara
wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa
wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.
Wajumbe wa kamati ya Ardhi,Maliasili
na Utalii waliozungumza na Clouds Tv ,Sebastian Kapufi na Dkt Godwin Mollel
wamesema hatua ya wafugaji hao kuzuia msafara wa kamati ililenga kuvuruga ziara
hiyo.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge
ya Ardhi ,Maliasili na Utalii wakiwemo wataalamu na wanasheria imewasili
Loliondo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi,Atashasta Nditiye na kufanya
ziara ya kutembelea eneo lenye ukubwa kilomita 1500 za mraba linalokusudiwa
kurejeshwa katika hifadhi .
Eneo hili linatajwa kuwa na vyanzo
vingi vya maji yanavyotiririka katika mto Gurumeti unaopita katika Hifadhi
ya taifa ya Serengeti ambao ni muhimu kiikolojia kutokana na maji yake kutumiwa
na wanyama pori katika hifadhi hiyo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment