Promota wa mchezo wa masumbwi Bob Arum, amethibitisha
uwezekano wa magwiji wawili wa mchezo huo Manny Pacquiao pamoja na Floyd
Mayweather Junior, kupanda ulingoni baadae mwaka
huu.
Arum, amethibitisha uwezekano huo baada ya kuweka hadharani taarifa za kukubali kwa Manny Pacquiao kupanda ulingoni kupitia kwa muwakilishi wake.
Promota huyo amesema muwakilishi wa bondia huyo kutoka nchini Philippines amekubali dili ambalo litakamilisha mpango wake wa kutimiza lengo la kukabiliana na Mayweather ambae alikua akimuhutaji kwa miaka kadhaa iliyopita.
Hata hivyo Bob Arum, amesema anaendelea na mazungumzo na upande wa Mayweather na anaamini atakubaliana na dili la kupanda ulingoni ambalo litaambatana na harakati za kusainiwa kwa mkataba wa pambano hilo.
Mwishoni mwa juma lililopita taarifa kutoka katika vyombo mbali mbali vya habari vya mjini Las Vegas zilieleza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa pambano la magwiji hao likafanyika katika ukumbi wa MGM Grand Garden May mbili mwaka huu.